• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Tehama na Uhusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Afya

Wilaya ina vituo 43 vya kutolea huduma za afya, vikiwemo Vituo vya Afya 6 na Zahanati 37, kati ya zahanati hizi 2 zinamilikiwa na mashirika ya dini.  Wilaya inaendelea na ujenzi wa zahanati 2 katika vijiji vya Chonde na Mayamaya. Pia, Wilaya inapanua Kituo cha Afya Bahi ili kuweza kutoa huduma za upasuaji wa dharura.  Huduma za afya zinatolewa kwa kuzingatia maeneo muhimu ya afya ya Uzazi na Mtoto, Afya ya Kinga (Udhibiti na Kinga ya Magonjwa kwa Jamii), Udhibiti wa magonjwa ya eneo husika (maalum) kama vikope na kichocho. Uimarishaji wa huduma za kiutawala, miundombinu, vifaa na dawa (tiba). Wilaya imefanikiwa kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi kutoka 9 mwaka 2000 hadi kufikia vifo 4 mwaka 2016. Pia, katika kipindi hiki, Wilaya imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka vifo 40 hadi kufikia vifo 12 mwaka 2016.

Aidha, sekta ya afya bado ina upungufu mkubwa wa watumishi kulingana na ikama.  Hadi sasa kuna jumla ya watumishi 369 kati ya 779 wanaohitajika na hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 410.

Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Wilaya inaupa kipaumbele ili kuboresha afya za wakazi wake na ilijiwekea lengo la kusajili kaya 15,269 (31%) kati ya kaya 49,554 za Wilaya kwa miaka mitatu (2015 hadi 2017) chini ya mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS). Katika kipindi hicho Wilaya imefanikiwa kusajili kaya 8,190 (54%) ya lengo, ambapo shilingi 184,270,000.00 zimekusanywa. Umuhimu wa kujiunga na mfuko huu bado utaendelea kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vya Kiserikali, vituo vya Afya na Zahanati.

Elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI inatolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ikisisitiza njia mbalimbali za ueneaji, jinsi ya kujikinga pamoja na umuhimu wa mabadiliko ya tabia kwa jamii hasa vijana ambao ndio waathirika wakubwa katika jamii yetu. Kampeni dhidi ya UKIMWI inaendeshwa kwa kutoa elimu na upimaji wa VVU wakati wa matukio ya sikukuu za kitaifa na kimataifa ikijumuisha  sikukuu ya wakulima, siku ya UKIMWI duniani.

Makundi maalum yanashirikishwa katika kampeni, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa baa, wakunga wa jadi, viongozi wa dini, kisiasa na wasanii (vikundi vya ngoma). Wazazi hupatiwa elimu siku za kliniki ya mama na mtoto. Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ni wadau muhimu katika kutoa elimu na huduma dhidi ya UKIMWI. Viongozi wa dini wanatoa elimu kwa waumini, pamoja na viongozi wa kisiasa na jamii yote kupitia mikutano ya hadhara.

Wananchi waliopima kwa hiari kati ya Januari hadi Desemba, 2015 ni 15,435 (Me 5,893 na Ke 9,542). Waliogundulika kuwa na maambukizi ya VVU ni 377 (Me 143, Ke 234) sawa na 2.4%. Wilaya ina vituo 5 vinavyotoa huduma ya dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV’s), ambapo wagonjwa 1,420 wanahudumiwa kati ya wagonjwa 2,000 walioandikishwa. Vituo hivyo ni Babayu, Bahi, Chipanga, Mtitaa na Mundemu.  Mpango wa kuongeza vituo vingine unaendelea, huduma mseto za Kifua Kikuu na UKIMWI zimeanzishwa na kuimarishwa ambapo kati ya wagonjwa 91 wa Kifua Kikuu 11 wamegundulika kuwa na maambukizi ya VVU katika kipindi hicho.

Matangazo

  • Tangazo la Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani Kujadili Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 February 10, 2021
  • Tangazo la Kikao cha Baraza la Madiwani January 27, 2021
  • Tangazo la Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Wilaya ya Bahi December 18, 2020
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi za Kazi za Mtendaji wa Kijiji Daraja la III November 02, 2020
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mabati 780 Yanunuliwa, Mfuko wa Jimbo

    February 12, 2021
  • Baraza la Madiwani Lapitisha Bajeti ya Shilingi Bilioni 25

    February 12, 2021
  • Watakaonunua Ardhi, Wenye Leseni za Madini Ujenzi Kuchangia Elimu

    January 29, 2021
  • Mfuko wa Jimbo Kusaidia Ujenzi wa Madarasa, Zahanati

    January 28, 2021
  • Tazama Zote

Video

RC MAHENGE AZITAKA HALMASHAURI ZA JIJI LA DODOMA KUAINISHA FURSA ZA UWEKEZAJI.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma
  • Tovuti ya Ikulu

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 26 2961400

    Simu: +255 766 643 266

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa