• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Tehama na Uhusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Bahi Yazindua Rasmi Ujenzi Hospitali ya Wilaya

Imechapishwa: January 12th, 2019

Benton Nollo, Bahi 

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amezindua rasmi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bahi na kuuagiza uongozi wa Halmashauri pamoja na kamati zote zinazohusika na usimaminzi wa ujenzi wa mradi wa hospitali hiyo, kuhakikisha kuwa inakamilika ifikapo tarehe 30 Mei, 2019.

Munkunda alitoa agizo hilo tarehe 12 Januari 2019 wakati akizindua eneo linalotarajiwa kujengwa hospitali hiyo.

Alisema kutokana na maandalizi yote ya msingi ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ujenzi (Bati,Nondo na Mchanga) kuwa yameshakamilika hakuna sababu inayoweza kukwamisha ujenzi huo.

‘’Naagiza, nataka mradi huu kwa sababu kila kitu kipo tarehe 30 mwezi wa tano mwaka huu tuwe tumekwisha kamilisha majengo yote saba kwanini nasema hivyo , nasema hivyo nikiamini kabisa nguvu ya wananchi tunayo, maamuzi ya viongozi tayari yamekwisha fanywa kuanzia ngazi ya Mhe. Rais sasa tunasubiri nini, na taratibu zote za kisheria ambazo tulipaswa kuzifuata zimekwisha kamilika’’. Alieleza Munkunda.

Pia, Munkunda alizitahadharisha Kamati hizo pamoja na Vijana wa Jeshi la Akiba (Mgambo) kutoa taarifa kwa mtu yeyote au kamati yoyote itakayobainika ikihujumu fedha za ujenzi wa mradi huo endapo atabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Katika hatua nyingine, Munkunda aliwataka wananchi wa Wilaya ya Bahi kuwa na ushirikiano ili kuweza kuileta Bahi maendeleo kama ilivyo sera ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli.

‘’Niwaombe Ushirikiano huo mliouonyesha kwenye ujenzi wa Kituo chetu cha Afya na mpaka sasa tumeanza shughuli zote zinazofanyika kwenye kile kituo hasa upasuaji tuzifanye hapa kwenye hospitali yetu ya Wilaya’’. Alisema Munkunda.

Akizungumza awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Bahi, Leo Mavika alisema Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa Wilaya 68 zilizobahati kupewa fedha na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.

"Kwetu ni bahati si wilaya zote zimepata, tuwashukuru viongozi akiwemo Mhe. Rais na Serikali ya Awamu ya Tano kwa ujumla wake. Lakini, pia tumshukuru sana Mhe. Mbunge kwa juhudi zake kubwa za kuweza kufuatilia na kuipigania Wilaya ya Bahi kuweza kuipatia maendeleo". Alisema Mavika.

"Bahi tunayoizungumzia leo ina barabara za lami, ina Kituo cha Afya kinachofanya na upasuaji. Bahi tunayoizungumza leo sasa tunajenga Hospitali ya Wilaya kwangu mimi ambaye naikumbuka historia ya Bahi kwa miaka ya nyuma kwanza naona kama ni ndoto, pili naiona ni bahati na tatu naishia tu kumshukuru Mwenyezi Mungu, sasa nimeyasema haya ili kuwaomba Wananchi wa Bahi waweze kutoa ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha hospitali hii inajengwa na inakamilika kwa wakati". Alisema Mavika.

Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa Wilaya 68 nchini zilipokea fedha shilingi 1,500,000,000 (Bilioni moja na milioni mia tano) kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambayo kimsingi ikikamilika itapunguza adha ya wananchi wa Bahi kutumia gharama kubwa za matibabu Dodoma Mjini.

Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi 461 Waliochaguliwa Kusomeshwa na Mfuko wa Elimu wa Wilaya Bahi mwaka 2019 February 08, 2019
  • Tangazo la Wasiolipia Viwanja katika Mji wa Bahi "Kitalu J" February 07, 2019
  • Tazama Matokeo ya Kidato cha NNE 2018 na Matokeo Ya Upimaji ya Kidato cha Pili QT 2018 January 24, 2019
  • Matokeo ya Upimaji ya Kidato cha Pili 2018 January 04, 2019
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • 462 Waishio Mazingira Magumu Kusomeshwa Bahi

    February 08, 2019
  • "Wasiolipia Viwanja Kunyang'anywa"

    February 07, 2019
  • Mganga: Bahi Lazima Mabadiliko Yatokee

    February 06, 2019
  • Changamoto za Bahi Zamsononesha Waziri Mabula

    January 23, 2019
  • Tazama Zote

Video

RC MAHENGE AZITAKA HALMASHAURI ZA JIJI LA DODOMA KUAINISHA FURSA ZA UWEKEZAJI.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma
  • Tovuti ya Ikulu

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 26 2961400

    Simu: +255 767 545 154

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Watembeleaji

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa