• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia na Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC Munkunda: Someni kwa Bidii, Msikubali Kujifelisha

Imechapishwa: December 1st, 2020

Na Benton Nollo na Bernard Magawa DMC, Chidete

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chidete wameaswa kutojifeshilisha katika mitihani yao ya mwisho na badala yake wametakiwa kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao za baadaye.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Darasa la Sita shuleni hapo kutokana na kuibuka kwa baadhi ya wazazi kuwatishia watoto wenye uwezo mzuri darasani kufanya vibaya makusudi kwa kigezo cha kwamba hawana uwezo wa kuwasomesha pindi watakapofaulu.

Munkunda ameyasema hayo alipotembelea shule hiyo kukagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na nyumba moja ya mwalimu tarehe 01 Desemba 2020 ambapo aliridhishwa na ujenzi huo na kuagiza fundi wa madirisha ya vioo kukamilisha haraka.

“Wanangu kumekuwa na baadhi ya wazazi wenu wanawadanganya kwamba wakati mitihani ya taifa hasa wa Dara la Saba msifaulu kwa kuwa hawana uwezo wa kuwasomesha, msikubali hata kidogo Serikali yenu kwa sasa inatoa elimu bure kuanzia chekechea mpaka Kidato cha Nne hivyo hakuna kisingizio cha nyinyi kufanya vibaya.” Amesema Munkunda na kuongeza;

“Ndiyo maana hapa Chidete Serikali ya Awamu ya Tano imeleta shilingi milioni 85 kujenga miundombinu hii ambapo shilingi milioni 25 zimetolewa na Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo – EP4R na shilingi milioni 60 zimetolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania – TEA.”

Munkunda amewasisitiza wanafunzi hao kuzingatia masomo na kuacha utoro ili waweze kunufaika na elimu inayotolewa na serikali bila malipo.

“Watoto wazuri Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inawapenda watoto wote nchini ndiyo maana inaendelea kujenga miundombinu bora hadi vijijini ili muweze kufurahia mazingira mazuri ya kujifunzia hivyo, someni kwa bidii ili mfaulu na kufikia malengo yenu.”  Amesema Munkunda.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Mwanafunzi wa Darasa la Sita shuleni hapo, Paulina Motonyi ameishukuru Serikali kwa kuwajali na kuwajengea madarasa mazuri yaliyowekwa vioo na vigae hali inayowafanya wafurahi na kuona serikali yao inawajali na haina ubaguzi.

“Tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kujenga madarasa mazuri hadi shuleni kwetu…mwanzo madarasa kama haya tulikuwa tunayaona kwenye video kwa wenzetu mjini lakini leo na sisi tunayatumia.” Amesema Motonyi huku akifurahi.

Aidha, Munkunda pamoja na kufurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo aliiagiza kamati ya shule kwa kushirikiana na walimu waliopo kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa asilimia 100 ili majengo hayo yaweze kutumika kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (wa kwanza kulia) akizungumza na wanafunzi wa Darasa la Sita wa Shule ya Msingi Chidete wakati wa ziara yake alipotembelea shuleni hapo kukagua ujenzi wa madarasa manne na nyumba moja ya mwalimu tarehe 01 Desemba 2020. 

Mkaguzi wa Polisi, Edward Kazungu akiwatia moyo kusoma kwa bidii baadhi ya wanafunzi wa Darasa la Sita wa Shule ya Msingi Chidete ambao nao walisema wanatamani kuwa Askari wa Jeshi la Polisi kama alivyo yeye. 

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (wa pili kulia) akiwaagiza kamati ya shule kushirikiana na walimu waliopo kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa asilimia 100 ili majengo hayo yaweze kutumika kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA MFUPI HALMASHAURI YA WILAYA YA BAHI August 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI WAOMBAJI WA TENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA UCHAGUZI MKUU WA 29 OKTABA,2025. AWAMU YA PILI October 17, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI WAOMBAJI WA TENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA UCHAGUZI MKUU WA 29 OKTABA,2025. October 13, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI September 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI NGAZI YA WILAYA KWENYE UKAGUZI WA VIKUNDI VYA VIJANA, WANAWAKE NA WALEMAVU.

    October 02, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI (INEC) AWAPA NASAHA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA BAHI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 29,2025.

    September 24, 2025
  • TIMU YA MENEJIMENTI (CMT) YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BAHI NA OFISI YA MKUU WA WILAYA YAFANYA UKAGUZI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA FEDHA ZA SERIKALI KUU, WAHISANI NA MAPATO YA NDANI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026.

    September 22, 2025
  • ZIARA YA KATIBU TAWALA WA MKOA WA DODOMA WILAYA YA BAHI.

    September 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Jinsi ya kuomba uhamisho kwenye mfumo wa Utumishi
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • NECTA
  • Mfumo wa uhamisho kwa watumishi,Mikopo na Kupata Salary Slips
  • BAHI YOUTUBE CHANNELE
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitengo cha Ugavi na Manunuzi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 762077589

    Simu: +255 762077589

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa