• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Tehama na Uhusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Munkunda: Lishe Bora Muhimu kwa Afya ya Jamii

Imechapishwa: June 22nd, 2020

Na Benton Nollo, Bahi

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amesema ili jamii iweze kushiriki vema katika shughuli mbalimbali za maendeleo ni lazima iwe na afya njema, ambayo  hupatikana kwa mtu kuwa na lishe bora.

Munkunda ameyasema hayo wakati anafunga kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.

Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza Wataalam wa Afya wanaotoa huduma vituoni na Watoa Huduma Ngazi ya Jamii kwa kushirikiana vema na Jukwaa la Lishe Tanzania - PANITA kupitia Mradi wa Lishe Endelevu, wameweza kutekeleza Afua tisa (9) za mkataba huo kwa asilimia 81.7 katika kipindi hicho.

"Suala la lishe katika Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa vipaumbele vyetu kwani tunaamini ili jamii iweze kushiriki vema katika shughuli za kujiletea maendeleo na kukuza uchumi ni lazima iwe na afya njema na Afya njema inatokana na lishe bora". Anasema Munkunda.

Munkunda amesema kuwa hata tarehe 29 Juni 2020 shule zitakapofunguliwa, wilaya imeweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni ili waweze kumudu vizuri masomo yao.

Pia, Munkunda ametoa wito kwa akina mama wajawazito kutumia vidonge vya kuongeza damu lakini pia Wataalam wa Afya waendelee kutoa unasihi wa lishe  kwa wazazi au walezi wa watoto wenye umri kati ya miezi 0 hadi 23.

Kadhalika, amewasihi kuèndelea kutoa matone ya Vitamini 'A' kwa watoto wenye umri  wa  miezi 6 hadi 59.

Munkunda pia, amewahimiza Wataalam hao kuendelea kuwaibua watoto wenye utapiamlo mkali ili waweze kupatiwa matibabu.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Dkt. Philipina Philipo ameushukuru Uongozi wa Jukwaa la Lishe kwa kushirikiana vema na Wilaya ya Bahi kutekeleza maazimio ya Mkataba wa Lishe.

 Naye Mkurugenzi wa Mtendaji wa PANITA, Tumaini Mikindo ameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Bahi kwa kutekeleza maazimio hayo na ameiomba Halmashauri kuendelea kufanya ukaguzi wa vyakula katika maeneo ya biashara na kutoa fedha kupitia mapato ya ndani kutekeleza shughuli za lishe.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Dkt. Philipina Philipo akizungumza wakati kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Lishe Tanzania - PANITA, Tumaini Mikindo akizungumza wakati kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.

Mratibu wa Programu wa Jukwaa la Lishe Tanzania - PANITA, Jane Msagati akizungumza wakati kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.

Wajumbe wa Kamati ya Lishe Wilaya ya Bahi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanahamisi Munkunda (hayupo pichani) wakati akifunga kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (wa pili kushoto waliokaa), Afisa Lishe Mkoa wa Dodoma, Heriet Carin (wa pili kulia waliokaa), Mganga Mkuu Wilaya ya Bahi, Dkt. Philipina Philipo (wa kwanza kulia waliokaa) Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Lishe Tanzania (wa kwanza kushoto waliokaa) na Wajumbe wa Kamati ya Lishe Wilaya ya Bahi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufungwa kwa kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020. (Picha zote na Benton Nollo)

Matangazo

  • Tangazo la Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Wilaya ya Bahi December 18, 2020
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi za Kazi za Mtendaji wa Kijiji Daraja la III November 02, 2020
  • Tangazo la Walioteuliwa kuwa Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi na Makarani Waongozaji wa Vituo vya Kupigia Kura Uchaguzi Mkuu 2020 October 17, 2020
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Kazi za Muda October 07, 2020
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Jamii Yashauriwa Kuacha Ukatili

    December 17, 2020
  • Rasmi Ngano Kulimwa Bahi

    December 15, 2020
  • DC Munkunda: Madiwani Shirikianeni Kutatua Kero za Wananchi

    December 14, 2020
  • DC Munkunda Akabidhi Vifaa vya Milioni 10.8

    December 01, 2020
  • Tazama Zote

Video

RC MAHENGE AZITAKA HALMASHAURI ZA JIJI LA DODOMA KUAINISHA FURSA ZA UWEKEZAJI.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma
  • Tovuti ya Ikulu

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 26 2961400

    Simu: +255 766 643 266

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa