Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri ya Wilaya ya Bahi anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wotewalioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 26/09/2024 hadi 01/10/2024 nahatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenyeusaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
Usaili utafanyika kuanzia tarehe 26/09/2024 hadi 01/10/2024 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hilimuda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,
Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI,
Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NAHAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhivigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji yatangazo husika.
10. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyetivyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili nambaya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili. KUONA ORODHA YA WALIOITWA KWENYE USAILI GUSA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI 2024.pdf
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa