• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia na Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Fedha,Utawala na Mpiango

KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO (FUM)

Majukumu ya jumla:

Kamati hii inawashirikisha wenyeviti wa Kamati zote za Kudumu na inapaswa kukutana kila mwezi mara moja. Aidha, madaraka ya Kamati hii ni kama ya Kamati zingine za Kudumu na hivyo hairuhusiwi kisheria kufanya kazi/majukumu ya Kamati zingine za Kudumu. Kwa ujumla, majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali ya Halmashauri kwa kupitia vikao vyake.

Majukumu Maalum ya Kamati:

  • Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato
  • Kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti na mpango wa Maendeleo kwenye Halmashauri ili kuidhinishwa na Halmashauri.
  • Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri, ukusanyaji wa mapato, kufuta madeni, na kuomba vibali Maalum kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
  • Kufikiria na, pale inapowezekana, kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu Sheria Ndogo na utendaji katika ngazi za chini za Halmashauri.
  • Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya fedha (re-allocation) yaliyopo katika makisio yaliyoidhinishwa na kuyapeleka kwa Halmashauri.
  • Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye Kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawasilisha kwenye Halmashauri.
  • Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauri mikopo yote ya Halmashauri.
  • Kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290.
  • Kupokea na kujadili taarifa za wakaguzi wa fedha na mali ya Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelekezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa, Sura ya 290.
  • Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za Halmashauri, kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Waziri na taratibu nyingine zitakazowekwa na Halmashauri;
  • Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususan kuhusu taratibu za fedha, ikiwa ni pamoja na mapitio ya mara kwa mara yanayohusu thamani ya fedha ambapo Kanuni mbalimbali za manunuzi ya mali na vifaa hutumika;
  • Kufikiria na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali, vinavyotolewa na Halmashauri;
  • Kufikiria mapendekezo ya Bajeti na Mipango ya Maendeleo ya kila Kamati ya Kudumu na kuiwasilisha kwenye Halmashauri ili kupata idhini;
  • Kushughulikia tofauti ya mapato na matumizi katika bajeti yote na kupendekeza hatua stahiki ya kuchukua kuondoa mapungufu katika mapato au ziada matumizi;
  • Kufikiria mapendekezo yote yanayohusu matumizi makubwa ya fedha kabla hayajawasilishwa kwenye Halmashauri ili kupata idhini;
  • Kupokea mahesabu ya mwaka ya Halmashauri na kuhakikisha taarifa ya mahesabu ya mwaka inawasilishwa kwa wakati kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
  • Kupitia na kuidhinisha mpango wa manunuzi wa Halmashauri kwa kuzingatia mpango wa Bajeti uliopitishwa na Halmashauri;
  • Kupitia taarifa ya kila robo mwaka kuhusu Manunuzi iliyowasilishwa na Afisa Masuuli;
  • Kusimamia utekelezaji wa mikataba ya Halmashauri kwa kukagua miradi inayotekelezwa na vifaa vilivyopokelewa;
  • Kumwelekeza Mkurugenzi kufanya manunuzi au ukaguzi wa huduma au vifaa vilivyonunuliwa ili kupata thamani halisi, itafanyika hivyo endapo itadhihirika kwamba, maelezo yaliyotolewa kuhusu manunuzi ya vifaa au huduma hayaridhishi;
  • Kuidhinisha majina ya wajumbe wa Bodi ya zabuni na wa Bodi zingine kwa mujibu wa Sheria husika;
  • Kushughulikia orodha ya wadaiwa wote itakayokayowasilishwa kwenye Kamati na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;
  • Kupendekeza njia na taratibu za kuondosha vifaa chakavu. Uondoshaji wa vifaa unaweza kufanyika kwa njia ya kuuza au kuviharibu;
  • Kujadili na kupitia taarifa za fedha za kila mwezi na kila robo mwaka;
  • Kupendekeza kwa Halmashauri hatua za kuchukua kuhusu kufuta madeni ya Halmashauri;
  • Kushughulikia Sera kuhusu kukopa na uwekezaji,
  • Kujadili na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali vinavyotozwa na Halmashauri,  
  • Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na Halmashauri nyingine.
  • Kurekebisha na kusimamia makusanyo na matumizi ya mapato ya vijiji na miji midogo kwa mujibu wa Sheria, Sura ya 287.
  • Kuteua wakaguzi wa fedha/mali za Serikali za Vijiji kwa mujibu wa Sheria, Sura ya 290.
  • Kujadili na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kuhusu mambo yote ya yanayohusu masuala ya ajira na kinidhamu ya wafanyakazi na watumishi.
  • Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu nyumba za Halmashauri.
  • Kupokea na kutoa uamuzi juu ya mapendekezo ya watumishi wanaokwenda masomoni.
  • Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi, ikiwa ni pamoja na mikopo, nyumba, usafiri, matibabu, rambirambi na motisha nyinginezo.
  • Kupitisha mapendekezo ya kuthibitisha watumishi kazini baada ya kumaliza kipindi cha majaribio kulingana na miundo husika ya utumishi.
  • kupendekeza Sheria Ndogo zinazohusu Kamati hii






Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO May 07, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI May 02, 2025
  • Mikopo ya Hazina Kwa Watumishi wa Umma October 27, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU (Limetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 8(1) February 20, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MHE.KHADIJA SHABANI TAYA (KEISHA) ACHANGIA HUDUMA ZA AFYA KWA KUTOA MASHUKA 20 HOSPITALI YA WILAYA YA BAHI.

    May 12, 2025
  • MAFUNZO YA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA KIELETRONIKI YAFANYIKA JIMBO LA BAHI

    May 14, 2025
  • DC JOACHIM NYINGO AKABIDHI VIFAA VYA SHULE VYA MILIONI 5.3

    May 06, 2025
  • MWENGE WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI MOJA MILIONI MIA TANO KUMI NA SABA LAKI NANE ELFU MIASITA THEMANINI NA NANE NUKTA SITA.(TSH.1,517,414,684.63) KATIKA WILAYA YA BAHI.

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Jinsi ya kuomba uhamisho kwenye mfumo wa Utumishi
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • NECTA
  • Mfumo wa uhamisho kwa watumishi,Mikopo na Kupata Salary Slips
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitengo cha Ugavi na Manunuzi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 762077589

    Simu: +255 762077589

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa