Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe (pichani katikati) amewaalika wananchi wote pamoja na watumishi wa umma leo tarehe 16/12/2023 kushiriki zoezi la upandaji miti katika Wilaya hiyo ambapo wananchi wengi pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji Bi.Zaina Mlawa (pichani kushoto) wamejitokeza kuitikia wito huo na kushiriki katika upandaji miti katika makao makuu ya Halmashauri hiyo. Mhe.Godwin Gondwe amesisitiza utunzwaji wa miche hiyo 1,500,000 ambayo imepandwa na itaendelea kupandwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa