Katika kikao kilichofanya leo Tarehe 16/01/2024 katika kata ya ibihwa iliyoko katika Halmshauri ya Wilaya ya Bahi, Mkurugenzi Mtendaji wa Bi.Zaina Mlawa amefanya kikao na watumishi mbalimbali waishio katika ya Ibihwa ikiwemo walimu,watendaji,maafisa ugani ,maafisa maendeleo ya jamii pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi pamoja na viongozi wao wakisiasa na kuwasihi kufuata taratibu kanuni na miongozo ya kiutumishi ikiwa ni pamoja na kudumisha ushirkiano na upendo na wanachi ambao ndio wenyeji wa watumishi hao. Akiongea katika kikao hicho Bi. Zaina Mlawa aliwataka watumishi pamoja na wanachi hao kusema kero zao wazi wazi za kiutumishi ambazo zingine zilitatuliwa papo hapo na zingine zilibebwa na kamati ya aliyoongozana nayo kwa utatutizi zaidi. Pia Bi.Zaina Mlawa aliwahakikisha watumishi kuwa serikali ya Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanyia kazi maoungufu yote ya kiutumishi hivyo kuwasihi watumishi waongeze bidi katika utendaji wao na nidhamu ya kauli kwa wananchi wanowahudumia ikiwa ni pamoja na kudumisha maadili kwa watumishi hao kuwa mfano kwani wao ni kioo kwa jamii inayowazunguka.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa