Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC imemtangaza mgombea Urais wa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli kuwa mshindi katika nafasi hiyo kwa zaidi ya asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa.
Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage alipokuwa akitangaza matokeo hayo katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Jaji Rufaa (Mst), Kaijage alimtangaza Dkt. John Magufuli wa CCM kuwa mshindi wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura zaidi 12,516,252 sawa na asilimia 84.4. “Kutokana na matokeo haya, namtangaza Dkt. Magufuli wa CCM, kuwa Rais mteule baada ya kuongoza kwa kupata kura nyingi kuliko wagombea wenzake” Jaji Rufaa (Mst), Kaijage.
Jaji Rufaa (Mst), Kaijage aliwataja wagombea wengine na kura zao kwenye mabano kuwa ni Queen Sendiga (ADC 7,627), Twalib Kadege (UPDP 6,194), Hashim Rungwe (CHAUMA 32,878), Mazrui Khalfan Mohamed (UMD 3,721), Seif Maalim Seif (AAFP 4,635) na Tundu Lissu (CHADEMA 1,933,271).
Wengine ni Mutamwega Mugahywa (SAU 14,922), Cecilia Mmanga (Demokrasia Makini 14,556), Maganja Jeremiah (NCCR Mageuzi 19,969), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF 72,885), Philipo Fumbo (DP 8,283) na Bernard Membe (ACT-Wazalendo 81,129).
Akiongelea idadi ya waliojiandikisha kupiga kura, alisema kuwa ni 29,754,699, wakati idadi ya waliopiga kura ilikuwa 15,091,950, ambapo kula halali ni 14,830,195 na kura zilizokataliwa ni 261,755.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa