(Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza jambo (Picha na www.globaplublishers,com.co.tz))
BENKI ya NMB imepunguza kiwango cha riba katika mikopo yake kwa wateja_kutoka asilimia 19 hadi 17 kwa wateja wanaokopa kupitia mishahara kwa waajiriwa wa mashirika ya umma na wale wa binafsi.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker amesema benki hiyo imechukua hatua hiyo ikiwa ni utaratibu kupunguza riba kwa wateja wake.
Alisema punguzo hilo limegusa viwango vyote vya mikopo kwa kutumia mishahara kutoka kiwango cha chini cha shilingi 200,000 hadi cha juu cha shilingi milioni 150 kutegemea mshahara wa mkopaji.
Aliongeza kuwa ili kujenga mazingira mazuri kwa wateja wao mikopo yao sasa inashughulikiwa ndani ya saa 24 hadi muhusika anapokea mkopo wake.
“Wateja wetu wengi wa mikopo wamekuwa wakiomba tupunguze riba za mikopo yetu jambo ambalo tumelizingatia kwa sasa na tumeongeza ofa ya gharama bure za kushughulikia mikopo hiyo kwa wiki sita kuanzia leo,” alisema Bi. Bussemaker.
Alifafanua kuwa NMB inasikiliza zaidi ushauri wa wateja wake na ndio maana sasa wameongeza muda wa marejesho ya mikopo kutoka kiwango cha chini cha miezi 60 hadi miezi 72 (sawa na miaka mitano hadi sita).
Ongezeko hilo la muda wa kulipa marejesho linaweza kuwanufaisha pia wadaiwa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), ambapo mkopaji anaweza kuzungumza na benki kisha ikalipa mkopo wote naye akaendelea kulipa taratibu kwa mujibu wa makubaliano na benki hiyo. (Chanzo na May 25, 2018 Chanzo na Denis Mtima, Grobal Publisher online)
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa