• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia na Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Shule, Vyuo Kuendelea Kufungwa

Imechapishwa: April 14th, 2020

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa amesema agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi hapo Serikali itakapotoa tamko jingine.  

Pia, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesitisha maadhimisho ya Sherehe za Muungano (Aprili 26) pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ili kuepuka msongamano na kuendelea kuzuia virusi vya corona visisambae zaidi.  

Waziri Mkuu ameyasema hayo tarehe 14 Aprili 2020 katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa ya Mapafu (Covid 19) unaotokana na Virusi vya Corona. Amesema hadi leo, nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na Virusi vya Corona ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wanne ambao wote wapo jijini Dar es Salaam.  Amesema Serikali bado haijatangaza kuhusu kufunguliwa kwa shule, vyuo na shughuli za michezo pamoja na misongamano isiyokuwa ya lazima. 

Hivyo, maeneo hayo yataendelea kusalia katika karantini na wanafunzi wote wandelee kubakia majumbani kwao.  Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza shilingi milioni 500 ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya Sherehe za Muungano zipelekwe kwenye Mfuko wa Kupambana na Covid 19 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pia, Waziri Mkuu amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuiunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona kwani janga hilo ni kubwa na wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti Na: 9921159801 yenye jina la National Relief Fund Electronic.  Kadhalika, Waziri Mkuu amesema elimu ya tahadhali ni muhimu ikaendelea kutolewa kwa wananchi ili waweze kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona. “Kama si lazima kutoka, wananchi waendelee kutulia majumbani mwao.” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa. 

Aidha, ameongeza kuwa, Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kusimamia utoaji wa elimu ya kujikinga na virusi hivyo hasa katika Mkoa wa Dar es Salaam ambao unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ikifuatiwa na Zanzibar.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO May 07, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI May 02, 2025
  • Mikopo ya Hazina Kwa Watumishi wa Umma October 27, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU (Limetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 8(1) February 20, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DC JOACHIM NYINGO AKABIDHI VIFAA VYA SHULE VYA MILIONI 5.3

    May 06, 2025
  • MWENGE WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI MOJA MILIONI MIA TANO KUMI NA SABA LAKI NANE ELFU MIASITA THEMANINI NA NANE NUKTA SITA.(TSH.1,517,414,684.63) KATIKA WILAYA YA BAHI.

    April 25, 2025
  • MKOA WA DODOMA WAPOKEA RASMI MWENGE WA UHURU 2025.

    April 20, 2025
  • KARUME DAY

    April 07, 2025
  • Tazama Zote

Video

Jinsi ya kuomba uhamisho kwenye mfumo wa Utumishi
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • NECTA
  • Mfumo wa uhamisho kwa watumishi,Mikopo na Kupata Salary Slips
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitengo cha Ugavi na Manunuzi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 762077589

    Simu: +255 762077589

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa