Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jumanne tarehe 08 Juni 2021 anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Wanawake wa Mkoa wa Dodoma.
Akitoa taarifa ya Mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema kuwa, kikao hicho kitafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa Wanawake wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kushiriki kikao hicho ili kupata fursa ya kumsikiliza Rais Samia.
Aidha, amewataka Wanawake waliopo mikoa mingine ya Tanzania kufuatilia Mkutano huo wa Rais Samia na Wanawake wa Mkoa wa Dodoma kupitia vyombo vya habari vikiwemo vituo vya luninga, magazeti, redio na mitandao ya kijamii.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 755 352 875
Simu: +255 689 571 881
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa