Tafadhali pakua Fomu hiyo kwa kubofya maandishi ya bluu hapa mbele FORM YA MAOMBI YA KUTAMBUA NA KURASIMISHA UJUZI.pdf
Pia, kwa uelewa zaidi soma maelezo yafuatayo hapo chini: -
MPANGO WA UTAMBUZI NA URASIMISHAJI UJUZI
Je wewe ni fundi ambaye hujapitia mafunzo chuoni na hivyo hauna cheti?
Je una uzoefu kwenye fani yako usiopungua miaka mitano?
Je umri wako hauzidi miaka 45?
Je unapata changamoto ya kujiajiri au kuajiriwa kutokana na kutokuwa na cheti cha ujuzi wako?
Je ungependa kuboresha ujuzi wako, utambuliwe na kurasimishwa ili upewe cheti kulingana na ujuzi wako?
Kama ndivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu kwakushirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inatekeleza awamu ya tatu ya Mpango wa Kutathmini na Kurasimisha Ujuzi uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo.
Katika mpango huu unayo fursa ya kufanyiwa tathmini ya ujuzi wako, kupewa mafunzo ya kuziba mapungufu yatakayobainika, kisha kutunukiwa cheti kitakachokusaidia kutambulika kwa ujuzi wako na hivyo kukupa fursa ya kuajiriwa, kujiajiri na kuajiri wengine au kuendelea na mafunzo ya ngazi za juu.
Fani zitakazohusika katika awamu hii ni Uashi, Useremala, Ufundi magari (makenika), Upishi, Uhudumu wa hoteli, baa na migahawa, Ufundi bomba, Unyooshaji bodi za magari, Umeme wa majumbani, Ushonaji na Uchomeleaji vyuma.
Ikiwa unakidhi vigezo vilivyotajwa hapo juu, unahimizwa kuchukua fomu ya maombi bila malipo katika ofisi ya Afisa Vijana/Afisa Maendeleo ya Jamii katika ofisi za Halmashauri iliyo karibu na wewe.
Pia fomu hizo zinapatikana bila malipo katika vyuo vyote vya VETA na katika tovuti zifuatazo:
• www.veta.go.tz
Au bonyeza hapa kupata fomu
Mwisho wa kuwasilisha fomu hizo ni tarehe 25 Juni, 2020.
Mchakato wote wa tathmini na urasimishaji wa ujuzi utagharamiwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU).
Hivyo, washiriki hawatalipia gharama yoyote.
Kwa taarifa zaidi, wasiliana na Mratibu wa Programu hii kwa barua pepe
bwire.ally@veta.go.tz, simu namba 0715 55 55 85
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu - VETA
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa