Huduma ya maji imeongezaka kutoka 34.0% mwaka 2013 na kufikia 38.3% mwezi Julai, 2016. Idadi ya watu wanaopata huduma ya maji safi na salama imefikia 84,890. Vyombo 25 vya watumiaji maji vimeanzishwa kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji vijijini. Thamani ya mifuko ya maji imeongezeka kutoka shilingi 60,000,000.00 mwaka 2013 na kufikia shilingi 139,683,024.37 hadi Desemba, 2016. Fedha hizi hutumika kwa ajili ya kuchangia ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji katika vijiji husika.
Katika mwaka wa fedha 2016/2017, Wilaya inaendelea kujenga miradi katika vijiji 2 vya Mundemu na Nguji. Pia, Wilaya imepokea kiasi cha shilingi 400,000,000.00 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kukamilisha uboreshaji huduma ya maji katika Mji wa Bahi kwa kutumia maji kutoka katika kijiji cha Mkakatika. Utekelezaji wa Mradi huu upo hatua ya usanifu. Mkakati wa Wilaya wa muda mrefu wa kuimarisha huduma ya maji katika Wilaya ya Bahi na vijiji vinavyoizunguka ni kupata maji kutoka kijiji cha Mbwasa Wilaya ya Manyoni. Kazi ya upembuzi yakinifu ya mradi huu inaendelea kwa gharama ya shilingi 307,000,000.00 kati ya fedha hizo Halmashauri imechangia shilingi 32,000,000.00 na Local Investment Climate (LIC) imechangia shilingi 275,000,000.00.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa