Dira, Mwelekeo na Huduma zitolewazo na Idara ya Ardhi na Maliasili katika Halmashuri ya Wilaya ya Bahi:
DIRA: Kuwa idara inayotoa huduma nzuri na Bora za Ardhi kwa kwa kufuata Sheria Kanuni na Taratibu na zenye matokeo.
MWELEKEO: Katika kutoa huduma Idara itahakikisha kuwa huduma zote zinatolewa kwa usawa, bila aina yote ya ubaguzi wala upendeleo na zitakuwa shirikishi.
HUDUMA ZITOLEWAZO NA IDARA
Huduma zinazotolewa na Idara ni hizi zifuatazo:
SEKTA YA ARDHI
Sekta ya Maliasili na Mazingira
Shughuli zilizotekelezwa kwa mwaka 2016/2017:-
(a) Ardhi
Wilaya imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali zinazohusu maendeleo ya ardhi, ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa Makao Makuu ya Wilaya, upimaji wa mipaka ya vijiji na upangaji wa matumizi bora ya ardhi. Aidha, katika kuhakikisha kuwa Makao Makuu ya Wilaya yanaendelezwa, kwa mwaka 2015/2016 jumla ya viwanja 420 vilipimwa na kumilikishwa kwa waombaji mbalimbali. Mchoro wa viwanja 405 umeidhinishwa na viwanja vitapimwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo wilaya imepanga kupima viwanja 500. Hadi sasa upimaji wa awali wa viwanja 74 umefanyika.
(b) Misitu (isiyohifadhiwa)
Kwa sasa Wilaya inaendelea na mpango wa kutambua na kupima maeneo ya misitu isiyohifadhiwa na Serikali Kuu ambayo yako chini ya Serikali za Vijiji vyote 59. Mkakati wa Wilaya ni kuhamasisha na kusimamia wananchi watenge hifadhi za misitu ya vijiji. Hadi sasa jumla ya vijiji 18 vimetenga maeneo kwa ajili ya hifadhi ya misitu.
(c ) Mazingira
Wilaya inaendelea na uoteshaji wa miche ya miti na kuisambaza vijijini na mashuleni hivyo kuweza kupandwa katika maeneo husika. Kwa kipindi cha 2015/2016, Wilaya imeotesha jumla ya miti 427,000 na kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya.
Changamoto kubwa tuliyonayo katika Sekta hii ni uwepo wa migogoro ya mipaka ya vijiji. Mgogoro mkubwa ni kati ya kijiji cha Mphangwe (Bahi) na kijiji cha Wiliko (Chamwino). Juhudi za kusuluhisha mgogoro huu zimefanyika bila mafanikio, na suala hilo Halmashauri imeiomba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kusaidie kusuluhisha mgogoro huu.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa