Kuratibu na kuhuisha upangaji na udhibiti wa mipango ya Idara mbalimbali za Halmashauri.
Kubuni, kuandaa na kutafsiri sera/miongozo mbalimbali ya Halmashauri.
Kuandaa hotuba, taarifa za ziara za viongozi na matukio mbalimbali ya Kiwilaya, Kimkoa na hata kitaifa kama vile Mwenge.
Kufuatilia, kushauri na kuandaa mikakati mbalimbali ya kushirikisha Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) na wadau mbalimbali wote wanaofanya kazi Wilayani kwa lengo la kuwashirikisha kikamilifu kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kushirikiana na Wakuu wa Idara na Vitengo katika kuandaa nyaraka za Kamati ya Bunge ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (LAAC).
Kuandaa nyaraka za majadiliano na mipango ya maendeleo kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na Mashirika ya Kimataifa na nchi wahisani.
Kuandaa ratiba ya utekelezaji wa kazi mbalimbali ‘’Action Plan’’ kutokana na Mpango Mkakati [Strategic plan].
Kuandaa taarifa ya ulinzi na usalama ya kila mwezi na kuiwasilisha sehemu husika kila mwezi.
Kuelekeza na kushauri uibuaji wa Miradi yenye tija kwa jamii hasa ngazi za Kata na Vijiji.
Kuichambua miradi kutokana na vipaumbele vya Halmashuari na miongozo ya sera za kitaifa kwenye mfumo wa kuandaa na kutoa taarifa za bajeti (Plan Rep)
Kuratibu uandaaji wa Mpango Mkakati wa Wilaya ‘’Strategic Plan’’
Kuandaa na kupitia taarifa za kila robo mwaka mfano Council Development Report (CDR) na kuziwasilisha sehemu husika.
Kuhuisha, Kuchambua na kutafsiri takwimu na taarifa mbalimbali.