Shughuli za ufugaji zinaendeshwa kwa mfumo huria zikijumuisha idadi ya ng’ombe 203,319 mbuzi 105,206 kondoo 56,496 punda 9,443 nguruwe 3,504 kuku 221,710 kanga 2,623 na bata 2,912. Juhudi za kuboresha ufugaji zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu na kizazi cha mifugo ya asili. Wilaya ina jumla ya majosho 16, kati ya hayo 7 yanafanya kazi.
Wilaya imeanzisha mpango wa kuvuna mifugo ili wafugaji wawe na maisha bora yenye tija na mifugo michache yenye ubora na kupitia mpango huu jumla ya wafugaji 60 wamehamasishwa. Aidha, jumla ya vikundi 21 vya wafugaji wa ng’ombe, mbuzi na kuku vimeundwa na wafugaji wenyewe kwa kushirikiana na maafisa ugani ili kuwezesha wafugaji kupata msaada wa mafunzo ya ufugaji bora kwa vitendo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa