Wilaya ina mtandao wa barabara zenye urefu wa km 704.6, kati ya hizo barabara za vijiji ni km 401.5, barabara za Wilaya ni km 279.5 na barabara za mjini km.23.6. Katika kipindi cha 2015/2016, km 90.23 zimefanyiwa matengenezo ambazo ni sawa na 14% ya barabara zilizohitaji matengenezo, mistari ya makalavati 36 yamejengwa na madaraja 4 yamejengwa. Vilevile ujenzi wa madaraja 2 makubwa kupitia mpango wa kuondoa vikwazo (Improving Rural Access in Tanzania) unaofadhiliwa na serikali ya Uingereza unaendelea.
Wilaya ina njia ya reli yenye urefu wa km30.2, mtandao wa barabara za Mkoa km 45, barabara kuu km 40 na mtandao wa mawasiliano ya simu na radio. Kwa sasa Wilaya inaendelea na mpango wake wa kufungua barabara mpya za vijiji kwa lengo la kuunganisha na Makao Makuu ya Wilaya. Pia Wilaya imeanza kutekeleza mpango wake wa kujenga barabara za lami Makao Makuu ya Wilaya kwa kuanza barabara ya Km. 0.9.
USAMBAZAJI UMEME VIJIJI:
Wilaya ya Bahi ina vijiji vinne (4) vyenye mtandao wa umeme kati ya vijiji 59 vilivyomo katika wilaya ambavyo ni Bahi Sokoni, Ibihwa, Ibugule na Mundemu.
Katika mwaka wa fedha 2015/2016 vijiji vingine vitatu (3) vya Mpamantwa, Nkhome na Mtitaa vimepatiwa umeme na mkandarasi wa DEM CONSTRUCTION ENG. LTD. ambaye alishinda tenda ya kusambaza umeme katika vijiji hivyo kupitia mpango wa REA.
Aidha, Vijiji vingine (8) vitawekewa umeme wa REA vikienda sanjari na ujenzi wa msongo wa KV 400 wa njia kuu itokayo Iringa kwenda Shinyanga. Vijiji hivyo ni Mwitikira, Chibelela, Mzogole, Nghulugano, Mnkola, Uhelela, Bahi Makulu na Kigwe.
Mpango wa REA umesaidia umeme jua kuwekwa kwenye majengo ya Taasisi nane (8) ambazo ni Chonama Sekondari, Zahanati ya Makanda, Babayu Sekondari, Zahanati ya Babayu, Chikopelo Sekondari, Zahanati ya Zejele, Zahanati ya Nghulugano na Magaga Sekondari.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa