Malengo ya Kilimo:
Katika msimu wa mwaka 2015/2016, Wilaya ilijiwekea malengo ya kulima hekta 167,870 kati ya hizo hekta 114,940 ni mazao ya chakula na hekta 52,870 mazao ya biashara. Aidha, kiuhalisia jumla ya Hekta 147,320 zilitumika kulima mazao ya chakula na biashara.
Matarajio ya mavuno yalikuwa Tani 139,122 za mazao ya chakula na Tani 57,780 za mazao ya biashara. Kwa mazao ya chakula ambayo ni (Mtama, Uwele, Mpunga, Muhogo mbichi, Kunde, Njugu mawe na Viazi vitamu) uzalishaji halisi zilitarajiwa kupatikana Tani 75,465.66. Mahitaji ya chakula kwa mwaka kwa wakazi wa Wilaya ya Bahi ni Tani 68,360.9. Hivyo Wilaya ingefanikiwa kuzalisha ziada ya Tani 7,104.76 za mazao ya chakula. Kwa mazao ya biashara ambayo ni (Ufuta, Alizeti na Karanga) uzalishaji halisi ni Tani 32,528.10.
Hata hivyo, katika mwaka wa 2015/2016 Wilaya ilivamiwa na ndege waharibifu wa mazao (Kwelea Kwelea) na kusababisha athari katika vijiji 25 kati ya 59. Tathimini iliyofanywa na kamati ya maafa ya Wilaya ilionesha Ekari 19,121.3 za mazao ya chakula ziliharibiwa vibaya. Wilaya kwa kushirikiana na kitengo cha udhibiti wadudu waharibifu kanda ya Kati iliweza kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na ndege hao. Pia Wilaya imewasilisha maombi maalumu ya mbegu za mazao ya Mtama, Mihogo na Viazi lishe katika kitengo cha maafa katika ofisi ya Waziri Mkuu ili kusaidiwa, wananchi waweze kupata mbegu kwa ajili ya msimu wa 2016/2017. Wilaya imefanikiwa kupata mbegu jumla ya kilo 4,135 za mtama aina ya macia na kilo 1000 za mpunga (Saro – 5) na zoezi la kuzisambaza katika vijiji husika limekamilika.
Kwa msimu wa mwaka huu 2016/2017 Wilaya imejiwekea malengo ya kulima hekta 157,226 na kuvuna Tani 249,299 za mazao ya chakula, Tani 72,000 mazao ya biashara na Tani 8,442 za mazao ya mbogamboga na matunda.
Wilaya imepokea fedha za mradi kutoka JICA Shilingi 413,000,000.00 ambazo zimetumika katika shughuli za ukarabati wa eneo la chanzo cha maji kwa ajili ya skimu za Mtazamo/Uhelela na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika tarehe 15/01/2017.
Aidha, katika msimu huu wa kilimo hali ya unyeshaji mvua imekuwa chini ya wastani kama inavyoonekana kwenye jedwali lifuatalo:-
Jedwali 1: Hali ya unyeshaji mvua katika wilaya ya Bahi kwa miezi 2.
Mwezi |
Kiasi (mm) |
Siku |
Desemba
|
48.6 |
3 |
Januari
|
33.9 |
2 |
Jumla
|
82.5 |
5 |
Sekta ya Ushirika:
Wilaya ina jumla ya vyama vya ushirika 25. Kati ya vyama hivyo, vyama vya Akiba na Mikopo ni 18 na Vyama vya Mazao ni 8 vikiwa na jumla ya wanachama 3,307 (wanaume 1,934 na wanawake 1,373). Lengo kuu la vyama hivi ni kuinua hali ya maisha ya wanachama kwa kuhamasisha wananchi kuweka akiba na kupata mikopo ya fedha kwa ajili ya kufanyia biashara na kununua pembejeo za Kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Vyama vya Akiba na Mikopo vimeongezeka kutoka 6 mwaka 2010 hadi 18 mwaka 2015/2016, Vyama vya mazao (AMCOS) kutoka 0 mpaka 7na vikundi 17 hadi 47 pamoja na wanachama kutoka 982 hadi kufikia 3,307.
Vilevile Hisa, Akiba na Amana za wanachama zimeongezeka; Idadi ya hisa za wanachama zimeongezeka kutoka shilingi 10,939,000.00 mwaka 2010 na kufikia shilingi 55,534,000.00 mwaka 2015/2016. Akiba za wanachama zimeongezeka kutoka shilingi 22,419,300.00 hadi kufikia 84,653,000.00 na amana za wanachama kwa sasa zipo shilingi 15,752,000.00. Jumla ya mikopo yenye thamani ya shilingi 276,643,642.00 imetolewa kwa wanachama wa SACCOS.
Pia, wanachama 102 wa AMCOS wamejiandikisha katika mfuko wa Jamii wa NSSF kwa ajili ya kupata mafao ya uzeeni na kupatiwa huduma za matibabu na mazishi.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa