Wilaya ina jumla ya madarasa 71 ya elimu ya awali kati ya lengo la madarasa 72. Shule ya Msingi Kigwe Viziwi haina darasa la awali kwa kuwa mfumo wao kwa wanafunzi hao huendeshwa kwa hatua ya I, II na III kabla ya kuanza darasa la kwanza. Lengo la uandikishaji mwaka kwa 2017 ni kuandikisha wanafunzi 10,378 (wasichana 5,255 na wavulana 5,123). Wanafunzi walioandikishwa ni 8,473 wakiwa ni wasichana 4,288 na wavulana 4,185 sawa na asilimia 81.64.
Elimu ya Msingi:
Jumla ya shule za msingi zilizopo ni 72 zenye wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la saba wapatao 31,564 kati yao wasichana ni 16,534 na wavulana ni 15,030. Walimu waliopo ni 654 (wanaume 351 na wanawake 281) sawa na 65% ya mahitaji ambayo ni walimu 1006. Aidha kuna Waratibu Elimu Kata 22, (wanaume 20 na wanawake 2).
Elimu ya MEMKWA:
Wilaya inavyo vituo 12 vya Mpango wa Elimu ya Msingi Kwa Walioikosa ambavyo vina jumla ya wanafunzi 478 kati yao wavulana ni 292 na wasichana ni 186
Elimu ya MUKEJA:
Wilaya ina vituo 51 vya MUKEJA ambavyo vina jumla ya wanakisomo 1,491. Kati yao 890 ni wanawake na wanaume ni 601.
Katika kipindi cha 2015/2016 hakuna nyumba za walimu zilizojengwa, vyumba 5 vya madarasa na matundu 48 ya vyoo yamejengwa kupitia nguvu za wananchi, fedha za ruzuku ya kuimarisha serikali za mitaa na wafadhili mbalimbali.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa