Leo tarehe 01 Septemba, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kimefanyika kikao kazi kilichohudhuriwa na walimu wakuu,Maafisa elimu kata pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo kwa ajili kujadili namna kutekeleza Miradi ya Maendeleo katika Shule za Msingi mbalimbali zinazojenga Madarasa yenye thamani ya Tsh. Bilioni moja milioni mia nane na laki mbili.
Ujenzi huo unahusisha shule kumi na nne (14) ambazo ni Chali Makulu,Nghulughano,Nyerere,Mindora,Makanda,Nholi,Bahi Makulu,Chibaya,Chilungulu,Nondwa,Mkondai,Mpamantwa,Mayamaya na Kusila.
Aidha Ujenzi wa Miradi hiyo unahusisha Ujenzi wa Madarasa,Matundu ya choo,pamoja na Ujenzi wa Shule mpya mbili ambazo ni Maya Maya na Mpaman
twa.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa