Leo, 24/09/2025 Jaji wa Rufaa Mhe. Jacob Mwambengele ambae ni Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ametembelea jimbo la Bahi na kukutana na Msimamizi wa uchahuzi katika jimbo la Bahi na wasimamizi wasaidizi, katika ziara hiyo ambapo aliwapa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia viapo vyao na kuepuka kuwa na upande (Upendeleo) katika kipindi hiki cha uchaguzi kama walivyoapa katika viapo vyao.
Aidha, amesistiza kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bahi Ndugu. William D. Mpangala kuhakikisha form namba 29 zinazo muwezesha mwananchi kupiga kura ya kumchagua Rais akiwa mahali popote zinatolea katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi ili kuepuka malalamiko ya watu kuhamishwa bila kuwa na taarifa.
Akiongea hayo katika ukumbi wa Halmashauri Mhe.Jaji Mwambengele alitaka kutembelea mahali ambapo vifaa vya uchaguzi vimehifadhiwa baada ya kupokelewa kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ili kujiridhisha kama hakuna mapungufu yoyote na baadae kutembelea mikutano ya kampeni vyama mbalimbali inayoendelea katika jimbo hilo la Bahi ili kuona kama kanuni na taratibu za uchaguzi zinafuatwa.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa