Leo Tarehe 17/09/2025 Mhe. Khatibu Malimi Kazungu Katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kufanya utambulisho kwa watumishi wa Halmashauri na Taasisi mbalimbali.
Ziara hiyo ya Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma imehudhuriwa na Wakuu wa idara na Vitengo,wakuu wa Taasisi, Maafisa Ugani, Watendaji wa Kata pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Ziara hiyo ya siku moja imefanyika katika ukumbimwa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
Aidha, Katika ziara hiyo Mhe.Katibu Malimi Kazungu ametoa maagizo yafuatayo kwa watumishi katika Wilaya hiyo: -
1.Watumishi wazingatie Dira ya 2050 katika utekelezaji wa Majukumu yao ya kila siku.
2.Watumishi kuzingatia sheria kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao.
3. Watumishi kuzingatia kwamba nchi inaongozwa kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
4.Lakini pia kuzingatia kwamba nchi imeridhia maazimio mbalimbali ya kimataifa (Sustainable Development Goals).
5.Kuwekeza katika kilimo cha korosho ili kuendelea kukuza Uchumi wa Mkoa wa Dodoma.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa