Katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mpinga, kata ya Mpinga, tarafa ya Bahi Wilaya ya Bah limefanyika zoezi la utoaji wa hati Miliki za Kimila 360 bure kwa Wananchi, zoezi hilo limeongozwa na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Thobias Nyingo akishirikiana na Wataalamu wa Ardhi kutoka Tume ya Taifa ya Upimaji Ardhi, ikiongozwa na Bi. Susana B. Mapunda.
Mhe. Mkuu wa Wilaya amewaasa wananchi na viongozi wote waliokabidhiwa Hati, kuzitunza sehemu salama, pia kuzitumia vema kama mtaji kujiletea Maendeleo yao. Wajihadhali na matapeli watao jaribu kwenda kuwarubuni.Wazitumie ofisi za Serikali ngazi ya kijiji, kata na Wilaya kupata Ushauri pale watakapoona inafaa ili wasiibiwe.
Aidha, zoezi hilo limehudhuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Comrade Masima, Mhe. Mbunge wa jimbo la Bahi Mhe. Keneth Nollo na Diwani wa kata ya Mpinga Mhe. Kudagana Ndalu.
Mkutano wa hadhara ulihudhuriwa na timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi na kutoka ofisi ya Mhe. Mkuu wa Wilaya pia aliambatana na Bi. Mwanamvua Bakar (Katibu Tawala wa Wilaya) na Bi. Zaina Mlawa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
Kupitia zoezi hilo Wananchi wa kijiji Cha Mpinga kwa furaha, Wameishukuru sana Serikali kwa kuendelea kuwajali, Wamemshukuru sana Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Upendo wake katika kulifanikisha Zoezi la ugawaji Hati za Kimila, wanamuombea Afya Njema na wanamuahidi Mitano Tena.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa