• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia na Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC Bahi na Dodoma Wamaliza Mgogoro wa Mpaka

Imechapishwa: March 29th, 2019

Na Benton Nollo, Bahi

Mgogoro wa mipaka uliodumu kwa miaka mitano katika Kata ya Zanka, Kitongoji cha Halo Wilayani Bahi umekwisha baada ya Wakuu wa Wilaya za Bahi na Dodoma kumaliza mkanganyiko uliokuwepo kwenye eneo hilo kwa muda mrefu.

Kutoka mwaka 2014 eneo hilo limekuwa likikabiliwa na mgogoro wa mpaka ambapo baadhi ya wananchi na viongozi wakijitangaza kutii mamlaka ya Wilaya ya Bahi na wengine wakitii Wilaya ya Dodoma Mjini.

Mkutano huo uliofanyika Machi 16, 2019 ukiongozwa na Wakuu wake wa Wilaya, Mwanahamisi Munkunda wa Bahi na Patrobas Katambi kwa upande wa Dodoma Mjini ambao waliongozana na wajumbe wa kamati za Ulinzi na Usalama pamoja na wataalamu wa ardhi ambao walithibitisha eneo hilo la Kitongoji cha Halo lipo ndani ya Wilaya ya Bahi kwa mujibu wa Sheria.

"Kwa muda mrefu kumekuwepo na malalamiko kwenye eneo hili la Halo juu ya mipaka, kesi nyingi zimeshakuja ofisini kwangu na nikazitolea maelekezo, tunafahamu kumekuwepo na viongozi wanaoshinikiza baadhi ya wananchi kulazimisha kuwa Manispaa ya Dodoma ilhali wapo Bahi, mnapaswa kutambua wote ni Watanzania na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli inagawa huduma sawa kwa wananchi wake wote hivyo ukiwa Bahi au Dodoma kote utahudumiwa sawa lakini lazima tufuate Sheria za Nchi ambazo zinaelekeza pia juu ya mipaka ya Wilaya na Mikoa yetu," alisema Katambi.

Katambi ameongeza kuwa mgogoro huo ulisababishwa na kutokuelewa ambapo vikao vingi vilikaa bila mafanikio na kuwataka wananchi kuelewa kuwa suala la mipaka haliamuliwa kwa utashi wa mtu bali sheria za Nchi.

Hiki ni kikao cha sita tunakaa baada ya vikao vingi kufanyika bila kuleta muafaka, nachosema sasa sio Mimi Katambi sheria iko hivi, mwenye mamlaka ya kugawa Nchi katika mikoa, wilaya, tarafa mpaka vitongoji ni Rais na sheria zilizotungwa na Bunge au GN,  ukisoma katiba yetu ya mwaka 1977 ibara ya 2(1) na (2), land act S.4, GN GDNEDC No 190 (2007), mamlaka ya miji (mgawanyo kata) GN No. 294 na sehemu ya 27 kata ya Chihanga na mipaka ya wakati huo manispaa ya Dodoma GN No 89 ya 1983 pamoja na ramani za mipaka utajua hakuna mgogoro wowote baina ya wilaya hizi mbili,"alisema Katambi.

Katambi aliongeza kuwa ni suala la kukosa uelewa au uchochezi wa makusudi unaofanywa kisiasa na kuwaonya wote kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kubadilisha au kuigawa Nchi isipokua Rais au sheria zilizotungwa na Bunge.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda aliwataka wananchi hao sasa kuungana na Serikali yao kufanya shughuli za kimaendeleo baada ya muafaka kupatikana na kuwaomba kushirikiana naye kuhakikisha Wilaya ya Bahi inasonga mbele na kuwa ya mfano kwa Wilaya nyingine.

"Sasa naamini leo kila mmoja ataondoka hapa akiwa ameridhika baada ya wataalamu wetu wote wa Dodoma na Bahi kutuonesha kuwa eneo hili la Halo lipo Bahi na hiyo ni kwa mujibu wa vipimo vya GN, niwatake sasa kuacha migogoro isiyo na lazima na kuungana na Serikali yenu katika kufanya kazi, tumuunge mkono Rais wetu Dkt. Magufuli kwa kufanya kazi na siyo kuchochea migogoro," alisema Munkunda.

Nao Jonathan Chibalango (Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayamaya kilichopo Wilaya ya Bahi), Keneth Makole (Mwenyekiti wa Kijiji cha Gawaye kilichopo Wilaya ya Dodoma) na Shaban Hassan Liaka ambaye ni mwananchi katika eneo hilo, kwa pamoja waliwashukuru Wakuu wa Wilaya hao kwa kufika wenyewe katika eneo hilo huku wakisema ni Mara ya kwanza kwa Wakuu wa Wilaya hizo mbili kufika kwenye eneo hilo na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mipaka yao ambapo kuahidi kutii mamlaka ya Wilaya ya Bahi kwa kushirikiana na Serikali yao kuleta maendeleo kama sehemu yao ya kumuunga mkono Rais Magufuli.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO May 07, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI May 02, 2025
  • Mikopo ya Hazina Kwa Watumishi wa Umma October 27, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU (Limetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 8(1) February 20, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DC JOACHIM NYINGO AKABIDHI VIFAA VYA SHULE VYA MILIONI 5.3

    May 06, 2025
  • MWENGE WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI MOJA MILIONI MIA TANO KUMI NA SABA LAKI NANE ELFU MIASITA THEMANINI NA NANE NUKTA SITA.(TSH.1,517,414,684.63) KATIKA WILAYA YA BAHI.

    April 25, 2025
  • MKOA WA DODOMA WAPOKEA RASMI MWENGE WA UHURU 2025.

    April 20, 2025
  • KARUME DAY

    April 07, 2025
  • Tazama Zote

Video

Jinsi ya kuomba uhamisho kwenye mfumo wa Utumishi
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • NECTA
  • Mfumo wa uhamisho kwa watumishi,Mikopo na Kupata Salary Slips
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitengo cha Ugavi na Manunuzi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 762077589

    Simu: +255 762077589

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa