Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango leo tarehe 15 /01/2024 ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Mhe.Pius Mwaluko na Katibu wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi.Zaina Mlawa pamoja na wajumbe wengine wa kamati hiyo na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ili tembelea Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneno mbalimbali ya Wilaya hiyo ikiwa ni juhudi za Uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan
Viongozi wa kamati hiyo Umetembelea na kukagua maendeleo ya miradi hiyo inayoendelea kutekelezwa katika katika kata ya Ibihwa ambapo kiasi cha shilingi milioni sitini(60,000,000) kilitolewa na serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa mdarasa matatu ya wanafunzi katika shule yamsingi ibihwa, akisoma taarifa ya mradi mwalimu mkuu wa shule ya msing Ibihwa Bw.Edward E. Sindilo ameishukuru serikali kwa kuleta fedha za mradi huo ambazo zimetatua kero ya msongamano wa wanafunzi katika shule hiyo, aidha amewashukuru wananchi kwa kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo.
Pia,ziara hiyo ilipata kutembelea miradi mingine kama vile mradi wa ujenzi wa madarasa matatu (3) katika shule ya msingi mundemu uliogharimu kiasi cha shiringi milioni sitini na mbili(60,000,000),ujenzi wa uzio katika shule ya wanafunzi wenye ulemavu kusikia kigwe uliogharimu kiasi cha shilingi 30,000,000 ,ujenzi wa matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi mapinduzi wenye thamani ya shilingi 6,000,000. pia ziara hiyo iliishia katika kata ya zanka ambako ujenzi wa mradi wa matundu ya vyoo Katika shule ya msingi zanka na zahanati ya zanka unaendelea kutekelezwa.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa