Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.GODWIN GONDWE akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Bahi Bi. ZAINA MLAWA amealika vyama vya wakulima wa mpunga (AMCOS) lengo lilikuwa ni kutoa elimu ya mikopo ya kilimo kwa skimu za mpunga ili wakulima waweze kuwa na matumizi sahihi ya mikopo hiyo,tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi likishirikisha wataalamu kutoka taasisi ya fedha ya NMB.
Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Bahi inajivunia kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha Mpunga aina ya SUPA BAHI kupitia vyama vya wakulima wa Mpunga (AMCOS) vinavyo jumuisha skimu kama vile MTAZAMO, NGUVUMALI, BAHI SOKONI, BAHI MAKULU na MATAJI.
Kilimo cha mpunga ni miongoni mwa shughuli za kiuchumi zinazofany wa na wananchi ndani ya Wilaya hiyo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa