Shirika la FARM Africa kwa kushirikiana na shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) wanaendelea na utekelezaji wa Miradi ya Kilimo Himilifu cha Mtama (CSAP II) na Vijna Kilimo Biashara (VKB) katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
Katika kuendelea kutekeleza shughuli zake, miradi hii iimetoa mafunzo mahususi ya Kuboresha mbinu za kilimo cha mazao ya Alizeti na Mtama (Good Agricultural practices –GAP) ili kuwaweka wakumila tayari kwa msimu kuanza kutumia mbinu bora za kilimo cha mazao hayo . mafunzo yatafanyika kwa awamu ambapo awamu ya kwanza ya mwaka 2023 Mafunzo yataanza kutolewa kwa vijiji 32 (10 VKB na 22 CSAP II) ambapo jumla ya wanufaika 2673 (1132 VKB na 1541 CSAP) watafikiwa.Vijiji vimechaguliwa kwa kuangalia vigezo vya idadi kubwa ya wanufaika ,fursa za viwanda vidogo vidogo vya kusindika alizeti na fursa za idadi ya wanunuzi.
Mkuu wa Idara Kilimo wa wilaya, Maafisa ughani na wakulima viongozi kutoka kwenye kila Kijiji husika wamehusika moja kwa moja katika mafunzo haya.Mafunzo hayo yamefanyika na yataendelea kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 755 352 875
Simu: +255 689 571 881
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa