Na Benton Nollo, Bahi
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amesema mauaji ya Mwalimu Heladius Lucas Mgaya, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chilingulu aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku tarehe 06 Aprili 2020 ni ukatili mkubwa ambao hautakiwi kufimbiwa macho.
Munkunda ameyasema hayo wakati wa ibada fupi ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mgaya iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 08 Aprili 2020.
Mkuu huyo wa Wilaya amewahakikishia ndugu wa Marehemu kuwa Mwalimu Mgaya alikuwa ni mtu mwema sana. Aidha, amesema tukio lililotokea ni ukatili kama ulivyo ukatili mwingine na kamwe haukubariki ambapo amewaomba kutambua kuwa Serikali ipo kazini na wahusika watachukuliwa hatua stahiki kwani kazi hiyo tayari imeshaanza.
“Mimi na Mkurugenzi baada ya kupata taarifa za tukio hili mara moja tulikwenda eneo la tukio ambapo tuliungana na viongozi ngazi ya kata na kiukweli tunakemea matukio maovu kama haya na ninaahidi kuwa wale wote waliohusika vyombo vya dola vinaendelea na kazi na sharia itachukua mkondo wake”. Anasema Munkunda na kuongeza;
“Msione kwamba mlituletea kijana wenu Mgaya kwa kumsomesha kwa gharama kubwa amekuja kututumikia sisi Wanabahi ndo tunawapa zawadi ya kumrudisha akiwa kwenye sanduku, hapana, hapana kabisa na sisi tutaendelea kupambana kama Serikali kuhakikisha kwamba hili lililompata mtumishi mwenzetu, sumu hii iwe mwisho kwa sababu inawezekana tusipoikomesha itaendelea kututafuna sisi wote, maana yake sisi wote ni watumishi wa serikali bila kujali wewe unatumika katika eneo gani”.
Munkunda amewatoa hofu na kuwasihi watumishi katika wilaya hiyo kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki kigumu ambapo Serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga amewasihi watumishi wasiogope ijapokuwa tukio lililompata mtumishi huyo linasikitisha na linasononesha sana kwani ni ukatili mkubwa aliofanyiwa mtumishi huyo.
“Tukio hili ukilitafakali kibinadamu mioyo yetu inaguswa sana na unaona kabisa kutokea kwake ni kukosekana kwa upendo na wahusika kutokuwa na hofu ya mungu…sisi kama serikali wajibu wetu ni kufuatilia watoto wote kwenda shule sasa hili kwa ndugu zetu wa Chilungulu wakati Mwalimu Mgaya akitekeleza hilo alionekana kuwa kero kwao”. Amesema Dkt. Mganga
Kadhalika, Dkt. Mganga amewaomba viongozi wa dini kubuni mbinu mpya ya kuokoa roho za watu zilizopotea kwani maumivu yanayosababishwa na watu wasio na hofu ya mungu ni makali sana.
“…Penye upendo hatutegemei kukuta kitu kama hiki, hii ni chuki ndiyo maana imesababisha tukio kama hili ambalo linasononesha sana”. Amesema Dkt. Mganga.
Mwalimu Heladius Lucas Mgaya alizaliwa tarehe 03 Septemba 1979 katika Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe. Aidha, aliajiriwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mwaka 2004 na mpaka anafariki alikuwa ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chilungulu, Kijiji cha Chilungulu Kata ya Mundemu wilayani Bahi.
PICHA NA MATUKIO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga akizungumza baada ya ibada fupi iliyofanyika kumuombea Marehemu Mwalimu Heladius Mgaya aliyeuawa na watu wasiojulikana wakati akirudi nyumbani kwake usiku tarehe 06 Aprili 2020 katika Kijiji cha Chilungulu. Ibada hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 08 Aprili 2020 kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kijiji cha Iwungilo, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akizungumza baada ya ibada fupi iliyofanyika kumuombea Marehemu Mwalimu Heladius Mgaya aliyeuawa na watu wasiojulikana wakati akirudi nyumbani kwake usiku tarehe 06 Aprili 2020 katika Kijiji cha Chilungulu. Ibada hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya hiyo tarehe 08 Aprili 2020 kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kijiji cha Iwungilo, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Bahi, Mohamed Msongo akisoma wasifu wa Marehemu Mwalimu Heladius Mgaya aliyeuawa na watu wasiojulikana wakati akirudi nyumbani kwake usiku tarehe 06 Aprili 2020 katika Kijiji cha Chilungulu. Wasifu huo umesomwa baada ya ibada ya kumuombea Marehemu ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 08 Aprili 2020 kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kijiji cha Iwungilo, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Katekista Henry Nchingu wa Kanisa Katoliki Bahi akiendesha ibada ya kumuombea Marehemu Mwalimu Heladius Mgaya aliyeuawa na watu wasiojulikana wakati akirudi nyumbani kwake usiku tarehe 06 Aprili 2020 katika Kijiji cha Chilungulu. Ibada hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya hiyo tarehe 08 Aprili 2020 kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kijiji cha Iwungilo, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Viongozi mbalimbali wakitoa salamu za pole kwa wafiwa na waombolezaji waliofika kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Mwalimu Heladius Mgaya aliyeuawa na watu wasiojulikana wakati akirudi nyumbani kwake usiku tarehe 06 Aprili 2020 katika Kijiji cha Chilungulu. Salamu hizo zilitolewa baada ya ibada ya kumuombea Marehemu iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 08 Aprili 2020 kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kijiji cha Iwungilo, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Bahi na waombolezaji wakitoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Mwalimu Heladius Mgaya aliyeuawa na watu wasiojulikana wakati akirudi nyumbani kwake usiku tarehe 06 Aprili 2020 katika Kijiji cha Chilungulu Kata ya Mundemu. Heshima hizo zimetolewa baada ya ibada ya kumuombea Marehemu iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 08 Aprili 2020 kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kijiji cha Iwungilo, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Ndugu na Mtoto wa Marehemu Mwalimu Heladius Mgaya aliyeuawa na watu wasiojulikana wakati akirudi nyumbani kwake usiku tarehe 06 Aprili 2020 katika Kijiji cha Chilungulu, Kata ya Mundemu wakilia kwa uchungu wakati wakitoa heshima zao za mwisho kwa mpendwa wao baada ya ibada fupi ya kumuombea Marehemu iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 08 Aprili 2020 kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kijiji cha Iwungilo, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Baba Mlezi wa Marehemu, Mwalimu Albert Yosef Mlowe akitoa shukrani kwa niaba ya Familia kwa viongozi wa Wilaya ya Bahi na waombolezaji waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Mwalimu Heladius Mgaya aliyeuawa na watu wasiojulikana wakati akirudi nyumbani kwake usiku tarehe 06 Aprili 2020 katika Kijiji cha Chilungulu, Kata ya Mundemu baada ya ibada ya kumuombea Marehemu iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 08 Aprili 2020 kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kijiji cha Iwungilo, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Baadhi ya Walimu wakitoa jeneza lenye mwili wa Marehemu Mwalimu Heladius Mgaya aliyeuawa na watu wasiojulikana wakati akirudi nyumbani kwake usiku tarehe 06 Aprili 2020 katika Kijiji cha Chilungulu, Kata ya Mundemu na kuupakia kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea kijijini kwao Iwungilo, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi . (Picha zote na Benton Nollo).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa