Na Benton Nollo, Bahi
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unatarajia kuzifikia kaya zaidi ya milioni 1.4 katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF III) Awamu ya Pili unaotarajia kuanza hivi karibuni.
Idadi hiyo ni ongezeko la kaya laki 3 ukilinganisha na kaya milioni 1.1 zilizokuwepo katika utekelezaji wa TASAF III Awamu ya Kwanza iliyomalizika.
Hayo yamesemwa na Mtaalam wa Utafiti kutoka TASAF, Tumpe Lukongo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa mafunzo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wawezeshaji wa Ngazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuhusiana na zoezi la uhakiki wa kaya maskini.
“TASAF III Awamu ya Kwanza ilifikia kaya kwa asilimia 70, sasa katika sasa katika awamu hii tunataka kuzifikia asilimia 30 zilizobaki.”Amesema Lukongo.
Alisema tathmini ya utekelezaji wa mpango uliopita inaonyesha kuwa dhamira ya Serikali ya kupunguza umaskini nchini imefikiwa.
“Takwimu zinaonyesha kwamba utekelezaji wa Mpango huo kwenye kipindi cha kwanza umechangia kupungua umaskini wa mahitaji ya msingi kwa kaya kwa asilimia 10 na kwa kaya maskini sana umaskini uliokithiri umepungua kwa asilimia 12”. Alieleza.
Lukongo alibainisha kuwa katika utekelezaji wa mpango huo awamu ya pili mkazo mkubwa utawekwa katika kuwezesha kaya zitakazoandikishwa kwenye mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato.
“Kipindi hiki cha pili tutahakikisha huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa ili kutoa huduma na kuendeleza rasilimali watoto hususan katika upatikanaji wa elimu na afya,”. Amesema Lukongo.
Alisema TASAF III itatekelezwa katika Halmashauri zote 185 za Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar kwenye vijiji, mitaa, shehia pamoja na vijiji, mitaa na shehia ambazo hazikupata nafasi katika utekelezaji wa mpango huo uliopita.
Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka TASAF, Grace Kibonde akitoa maelezo kuhusu Kipindi cha Pili cha Mpango wa TASAF III kwa Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wawezeshaji Ngazi ya Halmashauri tarehe 29 Julai 2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka TASAF, Grace Kibonde (wa kwanza kushoto) akiwaelekeza washiriki wa Mafunzo namna ya kutumia Vishkwambi kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa Walengwa wa Kaya Maskini katika Halmashaurinya Wilaya ya Bahi tarehe 29 Julai 2020. (Picha zote na Benton Nollo).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa