WAFUGAJI WILAYANI BAHI WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA CHANJO ZA MIFUGO KITAIFA.
Kupitia Mpango wa chanjo Kitaifa Mhe Mkuu wa Wilaya ya Bahi ndugu Joachim Thobias Nyingo akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi zaina Mfaume Mlawa pamoja na katibu Tawala wa Bahi (Mwanamvua Bakari) wameshiriki kikao cha uzinduzi wa chanjo za Mifugo wa aina tatu Kuku,Mbuzi na Ng'ombe.
Aidha chanjo hiyo imeelezwa kutolewa kwa Bei nafuu kama ifautavyo;Kuku watapatiwa chanjo bila gharama yoyote,Mbuzi mmoja kwa bei ya shilingi 300 na Ng'ombe kwa gharama ya shilingi 500.
Kikao hicho cha uzinduzi wa chanjo za Mifugo kimehudhuriwa na wafugaji wa Wilaya ya Bahi pamoja na wadau wa Mifugo.
Kupitia kikao hicho Mhe Mkuu wa Wilaya ya Bahi amesisitiza sana wafugaji wote kushiriki chanjo hiyo kwa maslai mapana ya afya ya Mifugo ili kuwezesha ustawi mzurii wa uchumi kupitia soko la Mifugo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa