Na Benton Nollo
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imechaguliwa kuwa sehemu utakapofanyika uzinduzi wa Vituo 51 vya Hali ya Hewa na Vituo 15 vya Haidrolojia, Kituo cha Oparesheni na Mawasiliano ya Dharura na Kanzidata ya Taifa ya Kuhifadhi Takwimu za Hali ya Hewa. Uzinduzi huo utafanywa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) tarehe 27 Juni, 2018 kuanzia saa 06:00 mchana, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma ikiwa ni kuhitimisha awamu ya Kwanza ya mradi.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ni moja kati ya wanufaika wa mradi huo ambapo Kituo cha Hali ya Hewa kinachojiendesha chenyewe, kilisimikwa. Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Mabadiliko ya Tabianchi na Uboreshaji wa Mifumo ya Tahadhari za Awali umekuwa ukitekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Julai, 2014 hadi Juni, 2018. Mradi huo unalenga kuimarisha uwezo wa nchi katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa, mabadiliko ya tabianchi, taarifa za haidrolojia, mifumo ya tahadhari ya awali na uwepo wa taarifa kwa ajili ya kukabiliani na hali mbaya ya hewa na kujiandaa kukabiliana na majanga au maafa yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa