Na Benton Nollo na Bernard Magawa (DMC), Bahi
Mbunge wa Jimbo la Bahi, Kenneth Nollo (Mb) amesema ofisi yake kupitia fedha za mfuko wa Jimbo imejipanga kuhakikisha inasaidia mabati yote ya kuezekea vyumba 12 vya madarasa na zahanati tatu ambapo majengo hayo ujenzi wake unaendelea hivi sasa.
Nollo ameyasema hayo tarehe 28 Januari 2021 katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 kilichoketi kwa mujibu wa sheria kujadili utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kwa kipindi hicho.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Mfuko wa Jimbo tumeona ni busara nasi tununue mabati yote ya vyumba 12 vya madarasa vinavyoendelea kujengwa ili kukamilisha haraka majengo hayo ambayo yatatoa fursa kwa watoto waliofaulu na kukosa nafasi za kujiunga na masomo ya sekondari nao wapate nafasi za kuanza masomo haraka iwezekanavyo, mabati hayo tumeyanunua kiwandani na yamegharimu shilingi milioni 25.” Amesema Nollo na kuongeza;
“Pia, Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unavyofahamu Halmashauri yetu ina maeneo ambayo hayana zahanati, hivyo tumetoa shilingi milioni 10 kwa kila eneo, katika Zahanati tatu zinazoendelea kujengwa ambazo ni Nchinila, Nguji na Chikopelo.”
Nollo amezitaja kata zitakazonufaika na mabati hayo kuwa ni Mpinga, Ilindi, Bahi, Chibelela na Mpamantwa.
Mbunge wa Jimbo la Bahi, Kenneth Nollo (Mb) akizungumza kwenye kikao hicho.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa