Benton Nollo na Benard Magawa, Bahi
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021, Luteni Josephine Mwambashi amezimezindua Mfumo madhubuti wa Usimamizi na Uendeshaji wa Vituo vya Kutolea Huduma za Afya – GoTHOMIS katika Hospitali mpya ya Wilaya ya Bahi ambayo ujenzi wake uliaza rasmi mwaka 2019 ambayo tayariL imeanza kutoa huduma za afya kwa wananchi wilayani humo.
Luteni Mwambashi amezindua mfumo huo tarehe 25 Julai 2021 ambao lengo lake ni kurahisisha utoaji wa huduma za afya na kuboresha usimamizi katika ukusanyaji wa mapato hospitalini hapo.
Akizungumza baada ya kuzinduliwa kwa mradi huo wa mfumo wa kielekroniki katika hospitali hiyo ambayo inahudumia wananchi wapatao 271,071, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amesema hospitali hiyo ina vifaa vya kutosha kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo mitungi ya gesi kwa ajili ya kukabiliana ya dharura za magonjwa ya njia ya hewa.
“Ndugu Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, hospitali hii pia ina kitengo maalumu cha kutoa huduma kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya na vimeundwa vikundi vya wanafunzi shuleni kwa ajili ya kuelimisha wanafunzi wenzao juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya.” Amesema Munkunda.
Naye, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Dkt. Phillipina Philipo akitoa taarifa juu ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wilayani humo amesema hali ya maambukizi imeshuka ukilinganisha na mwaka 2020.
“Tunatoa huduma za ushauri na kupima (CTC) katika vituo vya afya 6 na Zahanati 11 wilayani hapa, ambapo maambukizi ya Virusi vya Ukimwi yamepungua kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka 2020 na kufikia asilimia 2.1 kwa mwaka 2021, pia tunatoa huduma rafiki katika vituo 22 kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la UMATI.” Amesema Dkt. Phillipina.
Awali akisoma taarifa ya Mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Afisa TEHAMA na Mahusiano Wilaya ya Bahi, Benton Nollo amesema Mfumo huo ambao umefungwa katika majengo yote 7 ambayo yameanza kutoa huduma hospitalini hapo, umegharimu shilingi Milioni 42 hadi kukamilika kwake.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa