Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Selemani Jafo amesema Serikali imewawezesha Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata fedha na usafiri ili waweze kusimamia vizuri utoaji wa elimu katika maeneo yao.
Jafo ameyasema hayo wakati akielezea mafanikio ya sekta ya elimu katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma tarehe 4 Agosti 2020.
Waziri Jafo amesema “Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu wa Elimu Kata zamani walilipwa mshahara kama mshahara wa kwake yeye na haukuwa na tofauti na mwalimu mwingine. Hapakuwa na suala la fedha ya usimamizi kama Mwalimu Mkuu na Mratibu wa Elimu Kata. Mheshimiwa Rais akasema hapana, akatoa kitu kinaitwa posho ya madaraka. Leo hii Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi na Mkuu wa Shule ya Sekondari na Mratibu Elimu Kata wanapata ‘responsibility allawance’ kitu ambacho hakikuwepo awali”.
Waziri huyo amesema kuwa posho hiyo imewawezesha walimu hao kuweza kusimamia vizuri zaidi elimu katika maeneo yao ya kazi.
Akiongelea changamoto ya usafiri iliyokuwa ikiwakabili Waratibu wa Elimu Kata, Waziri Jafo amesema kuwa Rais aliamua kununua pikipiki kwa ajili ya kuwawesha kutekeleza majukumu yao.
“Kwa Waratibu wa Elimu Kata kwenda kufanya ufuatiliaji ilikuwa kazi kubwa kutokana na kuwa na eneo kubwa la kufanya kazi bila usafiri. Mheshimiwa Rais ameamua kununua pikipiki 3,909 kwa Waratibu Elimu Kata nchi nzima. Leo Mratibu Kata anakagua shule yake moja na kwenda shule nyingine. Leo hii Mratibu Elimu Kata ana pikipiki yake nzuri, ana posho yake ya madaraka, mambo siyo mabaya”. Amesema Waziri Jafo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa