Kutokana na kuchelewa kuanza kwa maadhimisho ya wakulima (Nanenane) mwaka 2020 katika baadhi ya Kanda kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (Corona), Serikali imetangaza kuongeza siku mbili za maadhimisho ya sherehe hizo.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea Banda la Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TABWA) kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Amesema kuwa kulingana na mahitaji ya sherehe za wakulima kujifunza mbinu bora za kilimo, wananchi ambao hawakupata fursa awali watatumia nafasi hiyo kujionea mbinu bora za kilimo, mifugo na uvuvi.
Amesema kuwa malengo makubwa ya sherehe hizo ni pamoja na kuwaunganisha wakulima, wafugaji, wavuvi na wanaushirika kusherehekea kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kuonesha teknolojia na zana bora za kilimo, mifugo na uvuvi.
Kadhalika, Waziri Hasunga amesema kuwa maonesho hayo yanatoa fursa ya kuwakutanisha wakulima, wavuvi na wafugaji na watoa huduma za fedha, bima, mawasiliano, taasisi za umma na binafsi.
Maonesho ya sherehe hizo yanafanyika katika kanda mbalimbali kwenye mikoa ya Mwanza, Tabora, Simiyu, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Arusha na Lindi.
Katika maonesho hayo wakulima, wafugaji na wavuvi wanahamasishwa kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo wametakiwa kuchagua viongozi bora wenye uwezo wa kuendeleza sekta ya kilimo.
Maonesho hayo yanachagizwa na Kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Chagua Viongozi Bora 2020".
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa