• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Tehama na Uhusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Baraza la Madiwani Lapitisha Bajeti ya Shilingi Bilioni 25

Imechapishwa: February 12th, 2021

Na Benton Nollo na Bernard Magawa (DMC), Bahi.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Bahi limepitisha Bajeti ya Halmashauri hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni 25 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Kikao maalum cha Baraza la Madiwani kimefanyika tarehe 12 Februari 2021 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Bahi ambapo Waheshimiwa Madiwani wameiomba Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani ihakikishe kuwa inakamilisha ujenzi wa maboma yote ya shule na zahanati yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi ili kurudisha imani kwao kutokana na majitoleo waliyoyafanya katika miradi hiyo.

Akizungumza katika Baraza hilo Diwani wa Kata ya Ibugule, Blandina Magawa amesema kwamba ili kuunga mkono juhudi na nguvu kazi za wananchi ni vema katika bajeti hiyo Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani ijikite zaidi kukamilisha maboma ya madarasa na zahanati yaliyopo kuliko kuanzisha miradi mipya hali ambayo itawapa moyo wananchi kujitoa zaidi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti katika kata yangu nina maboma matatu yalijengwa kwa nguvu za wananchi, madarasa mawili na maabara moja ambayo hayajamaliziwa, naiomba Serikali kupitia Halmashauri imalizie majengo haya ili turudishe imani kwa wananchi kwa sababu tuliwaahidi wananchi waanzishe halafu serikali itamalizia, lakini  inasikitisha majengo hayo yametelekezwa kwa muda mrefu sana.” Amesema Magawa.

Aidha, Baraza la Madiwani limeiagiza Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini - RUWASA kuhakikisha inakuwa na mipango inayotekelezeka katika kusogeza huduma za maji kwa wananchi na kuacha kuahidi mipango isiyo na matumaini  kwani inaleta usumbufu kwa baadhi ya viongozi wa maeneo husika.

Pia, Baraza limeiagiza ofisi ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini - TARURA kuhakikisha wanaimarisha miundombinu ya barabara vijijini ili ziweze kutumika kipindi chote cha mwaka kwani barabara nyingi zinaharibika inapofika kipindi cha masika.

Awali akiwasilisha Mpango wa Maendeleo na Bajeti  ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa niaba ya Mkurugenzi  Mtendaji  wa Wilaya hiyo,  Afisa Mipango wa Wilaya, Charles Mduma amesema bajeti hiyo imezingatia mambo yote muhimu ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo, Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa, Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020, Sheria ya Bajeti pamoja na maendeleo endelevu.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi inalenga kukusanya na kutumia shilingi milioni 25,084,770,216/= kutoka katika vyanzo mbalimbali.” Amesema Mduma.

Afisa Mipango huyo alifafanua kuwa mapato ya ndani ni shilingi bilioni 1,500,000,000/= (6%), Matumizi ya Kawaida shilingi bilioni 1,000,0024,609/= (4%), Mishahara shilingi bilioni 14,859,440,998/= (59%) na miradi ya maendeleo shilingi bilioni 7,725,304,609/= (31%).

 Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Mejiti amewasisitiza wajumbe kuhakikisha kuwa wao kama viongozi, wanasimamia na kudhibiti uanzishwaji wa makazi mapya mbali na huduma za jamii bila kufuata utaratibu badala yake wakae katika vijiji ambako Serikali imewekeza fedha nyingi kujenga miundombinu na huduma mbalimbali ikiwemo shule na zahanati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga akifafanua jambo wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Bahi kwa mwaka  fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 12 Februari 2021.

Afisa Mipango Wilaya ya Bahi, Charles Mduma akiwasilisha Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Bahi kwa mwaka  fedha 2021/2022 katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 12 Februari 2021.

Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Bahi, ASP Juma Solomoni akibu hoja ya Diwani wa Kata ya Chipanga, Masumbuko Kawindi (hayupo pichani) kuhusu kukiboresha Kituo cha Polisi cha Chipanga ili kiweze kutoa huduma bora kwa wananchi wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 12 Februari 2021.

Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakichangia hoja wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Bahi kwa mwaka  fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 12 Februari 2021.

Meneja wa TANESCO Wilaya ya Bahi, Bryceson Kitila akijibu baadhi ya hoja zinazohusu masuala ya umeme wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Bahi kwa mwaka  fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 12 Februari 2021.

Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini - TARURA, Mhandisi John Chalula akiwasilisha bajeti ya barabara wilayani humo wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Bahi kwa mwaka  fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 12 Februari 2021.

Mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Wilaya ya Bahi, Boniface Bihemu akijibu baadhi ya hoja zinazohusu masuala ya maji wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Bahi kwa mwaka  fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 12 Februari 2021.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bahi, Sterwart Masima akizungumza wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Bahi kwa mwaka  fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 12 Februari 2021.

Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia wasilisho la Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Bahi kwa mwaka  fedha 2021/2022 wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 12 Februari 2021. (Picha zote na Benton Nollo).

Matangazo

  • Tangazo la Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani Kujadili Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 February 10, 2021
  • Tangazo la Kikao cha Baraza la Madiwani January 27, 2021
  • Tangazo la Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Wilaya ya Bahi December 18, 2020
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi za Kazi za Mtendaji wa Kijiji Daraja la III November 02, 2020
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mabati 780 Yanunuliwa, Mfuko wa Jimbo

    February 12, 2021
  • Baraza la Madiwani Lapitisha Bajeti ya Shilingi Bilioni 25

    February 12, 2021
  • Watakaonunua Ardhi, Wenye Leseni za Madini Ujenzi Kuchangia Elimu

    January 29, 2021
  • Mfuko wa Jimbo Kusaidia Ujenzi wa Madarasa, Zahanati

    January 28, 2021
  • Tazama Zote

Video

RC MAHENGE AZITAKA HALMASHAURI ZA JIJI LA DODOMA KUAINISHA FURSA ZA UWEKEZAJI.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma
  • Tovuti ya Ikulu

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 26 2961400

    Simu: +255 766 643 266

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa