Tuesday 28th, November 2023
@Chimendeli Wilaya bahi
Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (ccm) Mhe. Mohamed Jawadu yatembelea Mradi wa shule Mpya ya Sekondari ya Chali (Chali Sekondari) iliyopo Kata ya Chali, tarafa ya Chipanga wilaya ya bahi mkoa wa Dodoma.
Aidha,mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi 544,255,626 mradi huo umekamilika tayari kwa matumizi na hatua za usajili wa shule hiyo mpya zinaendelea.
Pia, kamati hiyo ya Mkoa ikiongozwa na Mhe.Godwin Gondwe mkuu wa Wilaya ya Bahi ilitemebelea mradi mwingine wa ujenzi wa daraja Chimendeli kata ya Chikola, tarafa ya Chipanga Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma na mradi huo umegaharimu 403,236,666.67 chini ya Mkandarasi JP TRADERS kutoka Dar es salaam. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi machi,2024 mradi huo asimilia 53 mpaka sasa.Mradi huo ukikamilika utaunganisha Kijiji cha chimendeli na nghulugano na utarahisi usafiri kwa watumiaji wa njia inayouganishwa na Daraja hilo.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 755 352 875
Simu: +255 689 571 881
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa