Benton Nollo, Bahi
Mfuko wa Elimu Wilaya ya Bahi umepitisha majina ya wanafunzi 462 wanaoishi katika mazingira magumu wilayani humo ili waweze kugharamiwa sare, viatu na madaftari baada ya kuwa wamefaulu kujiunga na masomo ya Kidato cha Kwanza mwaka 2019 katika shule mbalimbali.
Majina hayo yamepitishwa kwenye kikao cha Kawaida cha Mfuko huo kilichoketi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 08 Februari, 2019 ambapo mwanafunzi mmoja kati ya hao anasoma Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Mundemu kwa kuwa mama yake anatatizo la kuongea (bubu) ambaye aliomba mtoto wake asaidiwe na mfuko huo.
Mfuko huo, umeidhinisha shilingi milioni 32.7 kati ya shilingi milioni 56 zilizopo katika mfuko huo zitumike kwa ajili ya kuwanunulia sare, viatu na madaftari. Aidha, wanafunzi watano wanaokwenda Shule ya Sekondari Mundemu wao pamoja na vifaa hivyo pia, watanunuliwa godoro moja kwa kila mmoja hivyo fedha zitakazotumika kwa ajili ya shughuli hiyo ni shilingi milioni 22.7 na shilingi milioni 10 zitatumika kwa ajili ya uhamasishaji na ufuatiliaji kwa kipindi cha mwaka mzima wa 2019.
Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Mfuko huo, Mhe. Donald Mejiti alitoa angalizo na kusisitiza kuwa manunuzi yote ya vifaa vilivyoidhinishwa na wajumbe kwa ajili ya wanafunzi hao, yafuate utaratibu wa manunuzi ya umma na isitolewe fedha taslimu kwa namna yoyote ile bali zipelekwe shuleni kwa idadi ya wanafunzi husika na wataalam walisimamie suala hiyo kikamilifu.
Kwa Upande wake Afisa Elimu Wilaya ya Bahi, Upendo Lweyemamu ambaye ndiye Katibu wa Mfuko huo aliwaeleza wajumbe kuwa majina hayo yaliwasilishwa na Waratibu Elimu Kata kutoka kwenye Kata zote 22 za Wilaya ya Bahi wakishirikiana na Walimu Wakuu katika maeneo husika na anaamini kuwa viongozi katika maeneo hayo wamehusika kuidhinisha upatikanaji wake.
Mfuko wa Elimu Wilaya ya Bahi ulianzishwa rasmi mwaka 2014 kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaofaulu vema masomo yao lakini wazazi au walezi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za kuwasomesha.
Kupata majina ya Wanafunzi hao bonyeza maandishi yenye rangi ya blue hapo chini:-
Habari Katika Picha:
Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Bahi, Mhe. Donald Mejiti (wa kwanza kulia) akiongoza kikao cha kawaida cha mfuko huo kilichoketi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 08 Februari, 2019 na kupitisha majina 462 ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wamefaulu kujiunga na masomo ya Kidato cha Kwanza katika shule mbalimbali za Wilaya ya Bahi kwa mwaka 2019. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda na wa kwanza kushoto ni Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bahi na Katibu wa Mfuko huo, Upendo Lweyemamu.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bahi ambaye pia ni Katibu wa Mfuko wa Elimu Wilayani humo, Upendo Lweyemamu akiongea wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Bahi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kigwe, Pascal Sijila akisisitiza jambo wakati wa kikao cha mfuko huo kilichoketi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 08 Februari, 2019 na kupitisha majina 462 ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wamefaulu kujiunga na masomo ya Kidato cha Kwanza katika shule mbalimbali za Wilaya ya Bahi kwa mwaka 2019.
Wajumbe wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Bahi, wakifuatilia na kupitia mambo kwa umakini wakati wa kikao cha mfuko huo kilichoketi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 08 Februari, 2019 na kupitisha majina 462 ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wamefaulu kujiunga na masomo ya Kidato cha Kwanza katika shule mbalimbali za Wilaya ya Bahi kwa mwaka 2019. (Pisha zote na Benton Nollo).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa