• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia na Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Airbus A220-300 Yatua Dodoma kwa Mara ya Kwanza

Imechapishwa: November 1st, 2020

Ndege kubwa aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132 na kutumia muda wa dakika 45 kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam, imetua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Dodoma baada ya uwanja huo kufanyiwa marekebisho makubwa kwa kuongezwa njia ya kutua na kurukia ndege kufikia urefu wa kilometa 2.8.

Ndege hiyo ya Serikali ya Tanzania iliyopewa jina la 'Ngorongoro Hapa Kazi' ilitua leo majira ya saa 10:43 jioni na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamurilo.

Akielezea zaidi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale amesema "Serikali iliamua kuongeza uwezo wa uwanja  huo  ili kuwe na ufanisi katika kuziendesha ndege zetu, kazi hii tulianza  Julai 2020 kwa gharama  ya Shilingi Bilioni 3.506"

Aidha, alisema kazi hiyo ilihusisha ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege hiyo. Kulilipwa fidia ya shilingi bilioni 5.8 kwa watu ili kupisha ujenzi huo na kazi iliyobaki ni kuweka taa ili kuruhusu ndege hiyo kutua hata usiku.

Akishiriki katika mapokezi hayo ya kihistoria kwa Jiji la Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kufanikisha ununuzi wa ndege na kuboresha wigo wa usafiri wa anga hadi kufikia Dodoma. Amesema hii ni fursa kwa watu wa Dodoma na duniani kote kwa kuwa fursa za urahisi wa usafiri na uwekezaji zinazidi kuongezeka Jijini Dodoma.

"Hii ni katika kuanza utekelezaji  wa mpango wetu wa kibiashara, tuna kituo kikuu Dar es Salaam, na tuna vituo vya kuunganisha ikiwepo Dodoma, Zanzibar, Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya. Hivyo ni vituo ambavyo tutaendelea kuongeza taratibu safari zetu za ndege kuunganisha na mikoa mingine na baadae na nchi za nje". Amesema Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi.

Naye Mkurugenzi Mkuu Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari amesema kuwa Uwanja wa Dodoma ulikuwa na uwezo wa kuruhusu kutua ndege yenye uwezo wa Q400 ambayo inabeba abiria 76, baada ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais na kwa kuwa Dodoma sasa imeshakuwa Makao Makuu, kazi ilifanyika ya kuongeza urefu wa barabara na kutengeneza taratibu za anga ambazo zina iwezesha ndege kubwa kama hii kutua na kuruka hapa chini salama ni mifumo inayotumia satelaiti.

Akimalizia Mkurugenzi huyo amewashukuru wadau wote kuanzia TANROADS, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Mamlaka ya viwanja vya usafiri wa anga pamoja na Wizara na Mheshimiwa Rais kwa mwongozo wake uliowawezesha kufanya kazi hiyo kwa haraka na ndege kubwa inaweza kutua.

Ndege aina ya Airbus A220-300 ikimwagiwa maji ya heshima na magari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kuikaribisha. Ndege hiyo imetua Dodoma kwa mara ya kwanza leo tarehe 31 Oktoba 2020.

Abiria waliosafiri na ndege ya Airbus A220-300 kutoka jijini Dar es Salaam wakishuka huku wakishuhudiwa na viongozi na baadhi ya wakazi wa Jiji la Dodoma leo tarehe 31 Oktoba 2020. 

Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi  akizungumza mara baada ya ndege aina ya Airbus A220-3000 kutua Jijini Dodoma kwa mara ya kwanza leo tarehe 31 Oktoba 2020.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO May 07, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI May 02, 2025
  • Mikopo ya Hazina Kwa Watumishi wa Umma October 27, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU (Limetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 8(1) February 20, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DC JOACHIM NYINGO AKABIDHI VIFAA VYA SHULE VYA MILIONI 5.3

    May 06, 2025
  • MWENGE WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI MOJA MILIONI MIA TANO KUMI NA SABA LAKI NANE ELFU MIASITA THEMANINI NA NANE NUKTA SITA.(TSH.1,517,414,684.63) KATIKA WILAYA YA BAHI.

    April 25, 2025
  • MKOA WA DODOMA WAPOKEA RASMI MWENGE WA UHURU 2025.

    April 20, 2025
  • KARUME DAY

    April 07, 2025
  • Tazama Zote

Video

Jinsi ya kuomba uhamisho kwenye mfumo wa Utumishi
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • NECTA
  • Mfumo wa uhamisho kwa watumishi,Mikopo na Kupata Salary Slips
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitengo cha Ugavi na Manunuzi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 762077589

    Simu: +255 762077589

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa