Na Benton Nollo
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imepokea msaada wa vifaa vya michezo kwa ajili ya Shule za Sekondari 20 ambavyo vimetolewa na Kampuni ya Coca Cola tarehe 27 Agosti, 2018 ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Kampuni hiyo imetoa jozi 40 za jezi na mipira 40 ambapo mipira 20 ni kwa ajili ya mpira wa miguu na mipira 20 ya mpira wa pete kupitia Mpango Kabambe wa kuinua michezo nchini Tanzania . Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya uongozi wa Kampuni hiyo Husna Hashimu alisema kuwa Kampuni ya Coca Cola imejipanga vema kushirikiana na Serikali katika kuinua na kukuza sekta ya michezo nchini na inaamini shuleni ndiko vilipo vipaji vingi vya michezo.
Akishukuru kwa niaba ya Halmashauri Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Bernadetha January alisema kuwa vifaa hivyo ni mkombozi katika sekta ya michezo kwa shule za sekondari kwani vitawapa motisha wanafunzi kupenda na kushiriki michezo hali ambayo itakuza vipaji walivyonavyo na kuwasaidia wafanye vizuri zaidi katika masomo yao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Bernadetha January (wa kwanza kushoto) akipokea mipira iliyotolewa na Kampuni ya Coca Cola na Mwakilishi wa Kampuni hiyo Husna Hashimu (wa kwanza kulia) kwa ajili ya Shule za Sekondari 20 ofisini kwake tarehe 27 Agosti, 2018. Katikati ni Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bahi, Patrick Gwivaha.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Bernadetha January (wa tatu kushoto) akipokea mipira iliyotolewa na Kampuni ya Coca Cola na Mwakilishi wa Kampuni hiyo Husna Hashimu (wa pili kulia) kwa ajili ya Shule za Sekondari 20 ofisini kwake tarehe 27 Agosti, 2018. Wa pili kushoto ni Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bahi, Patrick Gwivaha, Afisa Michezo, Yasint Kyera (wa kwanza kushoto) na Afisa Utamaduni, Rachel Mwitula. Picha zote na Benton Nollo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa