Mkuu wa Wilayaya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amewataka wakulima wa mpunga wa Skimu ya Bahi Sokoni kuchangia ushuru wa majaruba kama walivyokubaliana kwa lengo la kukarabati na kuendeleza miundombinu ya skimu hiyo. Munkunda aliyasema hayo wakati wa mkutano wake na wakulima hao uliofanyika uwanja wa Bahi Sokoni tarehe 08 Novemba, 2018.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Munkunda kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wakulima wa mpunga katika skimu hiyo, kuwa hawawezi kutoa ushuru huo kwa kuwa hawaoni faida kwani miundombinu haijaboreshwa.
Munkunda aliwataka wakulima hao kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na wao wenyewe kupitia vikao mbalimbali, ambayo ni kukusanya shilingi milioni 70 katika majaruba 3,500 ambapo ushuru kwa jaruba moja ni shilingi 20,000.00.
“Ndugu zangu nimekutana na ninyi leo kuwahamasisha mchangie ushuru wa shilingi 20,000.00 kwa jaruba kwani kwa taarifa zilizopo ofisini kwangu hivi ndivyo mlivyokubaliana. Hivyo, sioni kama ni jambo la busara kukiuka makubaliano wakati wa utekelezaji”. Alisema Munkunda.
Akifafanua mchanganuo wa ushuru huo wa shilingi 20,000.00 kwa jaruba katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Skimu ya Bahi Sokoni, Athuman Omar alieleza kuwa asilimia 50 inabaki kuhudumia skimu, asilimia 40 inakwenda Halmashauri na asilimia 10 inachukuliwa na Serikali ya Kijiji.
Mwenyekiti wa Skimu ya Bahi Sokoni, Athuman Omar akizungumza wakati wa mkutano huo.
Aidha, pamoja na mambo mengine wakulima hao katika kikao hicho walikubaliana kwamba kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2019 mgawanyo wa ushuru huo uwe kwamba asilimia 75 ibaki kwenye skimu, asilimia 15 iende Halmashauri na asilimia 10 ichukuliwe na Serikali ya Kijiji. Aidha, katika suala hilo Mkuu wa Wilaya alishauri kuwa mapendekezo hayo yapite kwenye vukao husika ili yapate ridhaa kwa ajili yautekelezaji.
Skimu ya Bahi Sokoni ni miongoni mwa skimu tano zilizopo Kata ya Bahi zinazofanya vizuri kwa uzalishaji wa zao la mpunga.
Baadhi ya wakulima wa mpunga wa Skimu ya Bahi Sokoni wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda (hayupo pichani) wakati wa mkutano alioufanya kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima hao tarehe 08 Novemba, 2018.
aadhi ya wakulima wa mpunga wa Skimu ya Bahi Sokoni wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda (hayupo pichani) wakati wa mkutano alioufanya kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima hao tarehe 08 Novemba, 2018. (Picha zote na Benton Nollo).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa