Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Joachim Nyingo tarehe 06 Mei 2025 amekabidhi vifaa vya Shure, Vitambaa , madaftari ,mashati ya shule zenye thamani ya shilingi
Milioni tano laki tatu ishirini na nne na mia nane.(50,324,800) Katika shule ya Bahi Sekondari Kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia duni.
Nyingo amekabidhi vifaa hivyo wakati akipokea taarifa ya Mfumo wa Elimu kwa Mwaka 2025, shuleni hapo iliyosomwa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Bahi Annette Nara
DC Nyingo amempongeza Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Donald Mejiti ( MNEC) kwa kuendelea kusisitiza na kusimamia swala la Elimu, unahaki ya kupongezwa sana kwenye Halmashauri yako imeweka utaratibu mzuri wa kutokumwacha mtoto asiende shule mtoto ni tunu mpe elimu bora, naipongeza Halmashauri kwa kutekeleza ndoto ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ataki mwanafunzi aachwe nyuma kwa sababu elimu ni ufunguo wa maisha ,mshike sana elimu,mpende sana elimu ,mtumikie sana elimu ,mkumbatie sana elimu. Nawapongeza sana waalimu kwa ujumla wenu kwa kazi nzuri na kubwa ambayo mnaifanya yakuendelea kuibeba elimu si tu kwenye Halmashauri yetu ya Wilaya ya Bahi bali Mkoa wetu wa Dodoma na Jamuhuri ya Muungano kwa ujumla, fedha zinazowekwa na serikali zinazoletwa na Dkt. Samia kwajili ya swala la elimu wenye dhamana ya kusimamia ni Halmashauri ikiongozwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya na Mkurugenzi lakini watekelezaji wa ile ndoto ya Mhe. Rais Samia ni waalimu ninawapongeza sana alisema DC Nyingo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri hiyo Zaina Mlawa amewapongeza wanafunzi wa Bahi Sekondari kwa usafi wa mazingira na sale za shule alisema uko mbele tunakondelea tutadumisha usafi wetu hata nyumbani, kipekee niwapongeze wazazi pamoja na waalimu kwa kuitikia wito wa kufika kwenye afla hiyo nyinyi tunawategemea sana ili tuweze kuibadilisha Bahi yetu kwa videndo kwamba Serikali imedhamiria, Halmashauri imedhamiria na viongozi wamedhamiria Bahi kuipeleka mbele Bahi ki elimu .
Sambamba na hilo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Donald Mejiti ( MNEC) alisema kipaji akijui kama mzazi ana uwezo tukasema hivi vipaji vya watoto tusiviache vikapotea mtoto alizaliwa na kipaji amefaulu vizuri sisi kama Halmashauri tumsaidie mzazi wake ambaye bahati mbaya mazingira ya kiuchumi siyo mazuri nyinyi watu wa Bahi naendelea kusema wananchi wa Bahi watoto wetu wanaakili sana uwenda wewe ukujua hapo nyuma ulichukulia tu kawaida lakini watoto wetu wanaakili mwaka jana wilaya yetu ya Bahi kwenye Halmashauri 184 nchi nzima Halmashauri yetu ya Wilaya ya Bahi ilishika nafasi ya pili Tanzania nzima hili siyo jambo dogo wazazi wa Bahi alisema .
Naye Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Bahi Annette Nara akitoa taarifa ya Mfumo wa Elimu kwa Mwaka 2025, Amesema kutokana na hali duni ya kiuchumi katika familia, baadhi ya wanafunzi huacha shule kwa sababu ya kukosa mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na sare ,vifaa vya shule kama vile madaftari,kalamu pamoja na magodoro kwa wale waliochaguliwa kwenda shule za bweni.
"Divisheni ya Elimu Sekondari Bahi Annette Nara amesema Baraza la Madiwani liliona changamoto hii na kukubaliana kuanzisha mfuko wa kusaidia na kuboresha Elimu Bahi kwa Lengo la kunusuru wanafunzi hawa kwa mstakabali wa maisha bora kwa wananchi wetu, Mfuko huu wa kusaidia na kuboresha Elimu ulianzishwa rasmi Oktoba 2014 kwa lengo la mfuko ni kusaidia wanafunzi watokao kwenye familia duni watasomeshwa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita.
Aidha, Mfuko wa Elimu kwa Mwaka 2025 umefanikiwa kusaidia wanafunzi 982 (Wavulana 403 na Wasichana 579) kuendelea na masomo katika shule mbalimbali za Sekondari. Baraza la madiwani limeendelea kufanya Shule ya Sekondari ya Mudemu kuwa shule Maalumu ya Sayansi kwa kuchagua wanafunzi wenye ufaulu mkubwa waliopata daraja A waliokosa nafasi za kwenda shule za bweni za Serikali, kwa kuzingatia ufaulu huo Baraza la Madiwani liliweka utaratibu wa kuchagua wanafunzi 120 (wavulana 60 na wasichana 60) kutoka Kata zote za Wilaya ya Bahi ili kujiunga na Shule ya Sekondari Mudemu. Pia Halmashauri imekuwa ikipeleka kiasi cha Tsh1,500,000 kila mwezi ikiwa ruzuku ya chakula kwa Wanafunzi hao .
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa