Benton Nollo, Chifutuka
Wananchi mkoani Dodoma wametakiwa kuchukua tahadhari ili kuepuka maafa yasiyo ya lazima katika kipindi hiki cha masika ambapo kuna mvua nyingi zinanyesha na kuleta athari ya uharibifu wa miundombinu mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge mara baada ya kutembelea miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Bahi mkoani Dodoma na kujionea athari za uharibifu zilizotokana na mvua hizo tarehe 02 Januari 2020.
“Viongozi waelezeni wananchi wasifanye mtihani wa kujaribu kuvuka katika makorongo wakati maji ni mengi yameweza kung’oa miti na kuondoa madaraja, hivyo tuwe waangalifu na tuchukue tahadhali katika kipindi hiki cha mvua zinazonyesha”. Amesema Dkt. Mahenge.
Aidha, Mahenge amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini - TARURA Mkoa wa Dodoma kuhakikisha ukarabati wa miundombinu hiyo unakamilika ndani ya siku 14 ili kurejesha huduma mbalimbali katika maeneo ya Tarafa za Bahi, Chipanga na Mwitikira ambapo baadhi ya miundombinu hiyo imeharibiwa na mvua hizo.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Bahi, Mhandisi John Chalula amesema wilaya hiyo tayari imeshapata zaidi ya shilingi milioni 150 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kukarabati miundombinu iliyoathirika wuilayani humo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuwa uongozi wa wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa huo watashikamana kwa pamoja ili ndani ya siku 14 alizozitoa huduma ya barabara kwa wananchi wa maeneo yaliyoadhiriwa ziendelee kama ilivyokuwa awali.
Maeneo yaliyoathiriwa na kutembelewa na Mkuu wa Mkoa ni Daraja Mfuto la Kigwe, Mzizima, Chikola, Mtitaa na Magaga ambayo yapo katika Tarafa za Bahi, Mwitikira na Chipanga.
Picha na Matukio:
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge akiwa pamoja na wataalam wa mkoa na viongozi wa Wilaya ya Bahi, katika ziara aliyoifanya tarehe 02 Januari 2020 wilayani humo ambapo alitembelea miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo. Pichani juu ni Daraja Mfuto la Kigwe.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge akiwa pamoja na wataalam wa mkoa na viongozi wa Wilaya ya Bahi, katika ziara aliyoifanya tarehe 02 Januari 2020 wilayani humo ambapo alitembelea miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo. Pichani juu ni Boksi Kalavati la Mtitaa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge akiwa pamoja na wataalam wa mkoa na viongozi wa Wilaya ya Bahi, katika ziara aliyoifanya tarehe 02 Januari 2020 wilayani humo ambapo alitembelea miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo. Pichani juu ni Boksi Kalavati la Chifutuka.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 687748878
Simu: +255 687748878
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa