Benton Nollo na Bernard Magawa (DMC), Bahi
Wito umetolewa kwa Walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani Bahi kuhakikisha wanaimarisha elimu ya dini katika shule wanazofundisha ambapo kwa kufanya hivyo watasaidia kuwajenga watoto kiimani na kuwakabidhi kwa Mungu ili waweze kuwa na mafanikio katika masomo yao.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga alipokuwa akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa elimu wilayani humo kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021 katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
Amesema, elimu ya dini itawafanya wanafunzi kuwa na hofu ya Mungu, wasikivu darasani kitu ambacho kitawasaidia kuwa na maadili mema na watakuwa na uwezo wa kufaulu vizuri katika mitihani pamoja na kujiepusha na mimba za utotoni.
“Pamoja na kufundisha kwa bidii lazima tumuombe Mungu atusaidie, twendeni tukawalee watoto kitaaluma na kiroho, hakikisha mtoto anayekuja shuleni kwako bila dini anapata huduma hiyo kupitia madhehebu mbalimbali kwani tunaamini baraka zinatoka kwa Mungu, sasa kama watoto hawatakuwa na mahusiano mazuri na Mungu watasaidiwa na nani.” Amesema Dkt. Mganga.
Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Donald Mejiti akizungumza kuhusiana na kutokomeza tatizo la ujauzito shuleni amesema kumekuwepo na uzungushwaji wa kesi mimba katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye kata na kuagiza kuanzishwa kwa mtandao maalumu utakaowajumuisha viongozi wote pamoja na walimu ili linapotokea tatizo mahali basi viongozi wote wafahamu kila hatua za kesi hiyo.
Awali, akitoa taarifa ya taaluma Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Bahi, Boniface Willison amewapongeza walimu pamoja na wadau mbalimbali kwa ushirikiano waliouonesha na kuifanya Halmashauri hiyo kuwa ya kwanza katika matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2020 kwa Mkoa wa Dodoma.
Pichani ni Wadau wa Elimu baada ya kikao cha wadau hao kufanyika tarehe 17 Februari 2021.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa