Halmashauri ya Wilaya ya Bahi yakabidhiwa Tuzo ya shukrani iliyowasilishwa kwa halmashauri hiyo kwa kutambuliwa kama bingwa kati ya mamlaka za serikali za mitaa kwa kutenga sehemu kubwa ya bajeti yake ya ununuzi kiasi cha asilimia 30 kwa ajili ya makundi maalum.Lengo ni kukuza ushirikishwaji na kutoa fursa kwa makundi hayo kwa kuwawezesha kushiriki katika shughuli za ununuzi kupitia mfumo wa kielektroniki wa NeST. Manunuzi haya yamefanyika kwa kipindi cha kuanzia julai 2023 hadi aprili 2025.Imewasilishwa na Mamlaka ya uthibiti wa ununuzi wa umma (PPRA).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa