Katibu Tawala Wilaya ya Bahi (Mwanamvua B. Muyongo) akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi (Bi. Albina William Mtumbuka) wametembelea Mradi uliofadhiliwa na kujengwa na Bank ya NMB ikiwa Ujenzi huo ni Shule ya Sekondary kwa ajili ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu, Mradi huu ambao unagharimu Billion 3.69 unajengwa katika Kata ya Bahi ikiwa lengo ni kuwasaidia Wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuwezeshwa kupata haki yao ya Msingi ya kupata elimu iliyo bora.
Mradi huu wa Shule ya Sekondary una jumla ya Madarasa sita (6),Mabweni Mawili (2) yenye uwezo wa Kulaza Wanafunzi 80 kila moja , Mabweni hayo mawili moja ni kwaajili ya Wanafunzi wa Kike na Moja kwaajili ya Wanafunzi wa Kiume , Maabara mbili (2) (Chemistry na Biology), Bwalo la Chakula pamoja na Jengo la Utawala. Mpaka sasa Mradi umefikia asilimia 65 na mara baada ya Mradi huo kukamilika kwa kiasi kikubwa utawarahisishia kundi kubwa la Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika suala la kupata elimu na ujifunzaji ili waweze kutimiza malengo yao ya baadae.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa