Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Godwin Gondwe akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Zaina Mlawa amefanya kikao na wenyeviti wa wafugaji 59 waliomo katika Wilaya hiyo na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili wafugaji na kujadiliana namna ya kutatua changamoto hizo.Aidha, kupitia kiikao hicho Mhe.Godwin Gondwe kwa kushirikiana na wataalamu wa Mifugo wametoa Elimu juu ya umuhimu wa chanjo za mifugo ili kuwa kinga mifugo dhidi ya magomjwa ya mapafu amabayo ni tishio kwa mifugo.
Kupitia kikao hicho pia kilichoshirikisha wenyeviti wa vijiji 59 vya walaya ya Bahi ,amewataka viongozi hao wa vijiji kujiunga na bima ya Afya ya iCHF (CHF Iliyoboreshwa) ikiwa ni pamoja kwashauri wawaelimishe wananchi wanaotoka katika vijiji vyao kujiunga na bima ya afya ilikupunguza gharama za matibabu na kulinda nguvu kazi ya taifa ili washiriki katika juhudi za kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa