Na Benton Nollo, Bahi
Mafundi 79 katika Wilaya ya Bahi watanufaika na Mpango wa Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi Uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo Awamu ya Tatu.
Kauli hiyo imetolewa na Frank Chanyika ambaye ni Mwalimu wa Chuo cha VETA Dodoma wakati akizungumza na mafundi hao walioitwa baada ya kukidhi vigezo, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Agosti 19, 2020.
Amesema Mpango huo ambao unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi - VETA unalenga kufanya tathmini, kurasimisha na kutunuku vyeti kwa mafundi wa fani mbalimbali waliopata Ujuzi nje ya mfumo rasmi wa mafunzo.
Aidha, Chanyika amefafanua kuwa kabla ya kupatiwa vyeti hivyo, mafundi hao watapata mafunzo rasmi na watajaribiwa ambapo gharama za majaribio hayo ambayo ni shilingi elfu kwa kila mmoja zinatolewa na Serikali.
Chanyika aliainisha fani zilizoombwa kurasimishwa kwa vijana hao kuwa ni Ufundi Seremala, Ufundi Bomba, Ufundi Uashi au Ujenzi, Ufundi unyooshaji magari, Upishi, Ufundi Umeme wa Nyumbani, Uhudumu wa Hoteli, Baa na migahawa, Ushonaji wa Nguo, Ufundi Magari na Uchomeleaji vyuma.
Frank Chanyika (kushoto) ambaye ni Mwalimu wa Chuo cha VETA Dodoma akizungumza na baadhi ya mafundi waliokidhi vigezo vya kushiriki mafunzo na kunufaika na Mpango wa Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi Uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo Awamu ya Tatu katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 20 Agosti 2020.
Picha za juu ni baadhi ya mafundi waliokidhi vigezo vya kushiriki mafunzo na kunufaika na Mpango wa Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi Uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo Awamu ya Tatu katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 20 Agosti 2020.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa