fisa Mwandikishaji wa Jimbo la Bahi Ndugu.William Dastan Mpangala awaapisha Waandishi wasaidizi na Bvr Kit Operators ambao watashiriki katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kidumu la Mpiga Kura awamu ya pili ambalo litaanza Rasmi Tarehe 16/05/2025 Jimbo la Bahi ambapo kata 22 za Jimbo la Bahi zitahusika.
Zoezi hili la awamu ya pili litahusisha wale ambao hawakujiandikisha katika zoezi lilopita kwasababu mbalimbali,waliopoteza viitambulisho vyao vya kupigia Kura,kuboresha taarifa zilizokosewa,kuhamishia taarifa lakini pia kufuta taarifa watu waliofariki. mzunguko wa pili wa uboreshaji wa Daftari awamu ya pili na uwekaji wazi wa Daftari la awali kwa muda wa siku Saba kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 22 Mei, 2025.
Mikoa ya mzunguko wa pili ni pamoja na Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida,Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.
Tukio Hilo limefanyika katika Ukumbi wa Side view Wilayani Bahi
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa